Na Bakari Madjeshi, Globu ya Jamii
Nyota
wa Kimataifa wa Argentina na Klabu ya Soka ya Barcelona ya Hispania,
Lionel Messi rasmi ametangazwa kuwa Mshindi wa Tuzo ya Ballon d'or ikiwa
ni mara ya 6 kutwaa Tuzo hiyo akiwa ni Mchezaji wa kwanza duniani
kuchukua kwa idadi hiyo katika historia ya Soka.
Messi
ametwaa tuzo hiyo inayotolewa na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) kwa
kushirikiana na Shirikisho la Soka nchini Ufaransa akitwaa mwaka 2009,
2010, 2011, 2012, 2015, 2019.
Katika
Tuzo hizo zilizotolewa mjini Paris nchini Ufaransa, Nyota wa Kimataifa
wa Marekani kwa upande wa Wanawake, Megan Rapinoe ametajwa katika Tuzo
hiyo ya Ballon d'or kwa mwaka huu wa 2019.
Matthijs
de Ligt wa Uhoalanzi na Klabu ya Juventus ametajwa katika Tuzo ya
Mchezaji Bora Kijana (Kopa Trophy 2019) wakati Jadon Sancho wa Borussia
Dortmund akitajwa kwenye nafasi ya Pili na Joao Felix wa Atletico Madrid
akitajwa katika nafasi ya tatu.
Golikipa
wa Kimataifa wa Brazil na Klabu ya Liverpool, Alisson Becker ametajwa
kuwa Kipa Bora wa Tuzo ya maalum iliyopewa Jina la Yachine Trophy 2019.
Wachezaji
3 kutoka Bara la Afrika waliingia katika 10 Bora zakuwania Tuzo hizo za
Ballon d'or ambao ni Riyad Mahrez, Sadio Mane na Mohammed Salah, wakati
huo Mane ametajwa katika nafasi ya Nne baada ya Mshindi kupatikana
ambaye ni Lionel Messi.
Sherehe
za Utoaji Tuzo hizo zilishereheshwa na Mchezaji wa zamani wa Kimataifa
wa Ivory Coast na Klabu ya Chelsea, Didier Drogba na Mwandishi wa Habari
wa Ufaransa, Mwanadada Sandy Heribert.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇