Sehemu
kubwa ya Watanzania hutegemea shughuli za kilimo kwa ajili ya chakula
na biashara na hivyo ni mchango mmojawapo wa uchumi wa Taifa.
Pia
Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha wakulima wananufaika
nma shughuli hizo za kilimo katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kwa
kilimo cha mazao tofauti tofauti
Hata
hivyo pamoja na juhudi hizo za Serikali bado wakulima wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa shughuli zao za kilimo na
hivyo kupata wakati mgumu.
Tanzania
ni miongoni mwa nchi zinazokabiliwa na changamoto ya uharibifu wa ardhi
ambayo inayoleta athari kwa kilimo hali inayochangia uzalishaji duni wa
chakula.
Hali
hiyo hutokana na shughuli za kibinadamu zinazofanyika zikiwemo zikiwemo
kuharibu vyanzo vya maji na ukataji miti kwa ajili ya kuni au uchomaji
wa mkaa hali inayochangia uharibifu wa mazingira.
Kutokana
na changamoto hizo, Ofisi ya Makamu wa Rais ambayo ina dhamana ya
usimamizi wa mazingira inaratibu na kutekeleza Mradi wa Kurejesha Ardhi
iliyoharibika na Kuongeza Usalama wa Chakula (LDFS) hapa nchini.
Mojawapo
ya malengo ya mradi huo ni kuboresha mifumo ya ikolojia ya kilimo
ambayo itawezesha kuongeza uzalishaji wa chakula na kuchangia kuboresha
mazingira katika wilaya husika.
Miongoni
mwa wilaya ambazo mradi huo unatekelewa ni nne za Tanzania Bara ambazo
mikoa yake iko kwenye mabano ni pamoja na Kondoa (Dodoma), Mkalama
(Singida), Nzega (Tabora) na Magu (Mwanza). Pia unatekelezwa katika
wilaya moja kwa upande wa Tanzania Zanzibar ambayo ni Micheweni
(Pemba).
Hivi
karibuni Ofisi ya Makamu wa Rais ilitoa mafunzo msasa ya uwezeshaji
kuhusu mashamba darasa kwa maafisa viungo wa mradi kutoka Wizara na timu
za uwezeshaji za wilaya wa mradi huo.
Mfunzo
hayo yatakuwa msaada mkubwa kwa maafisa hao ambao wataitumia elimu
waliyoipata katika kufanikisha uanzishaji wa mashamba darasa katika
maeneo ya mradi.
Tanzania
kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo wamekuwa wakitekeleza miradi
inayolenga kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na mifugo kwa kusogeza
karibu teknolojia kwa wakulima, lengo likiwa ni kuongeza usalama wa
chakula na kuongeza kipato cha jamii.
Hizi
ni juhudi za Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais inahusisha
uingizaji na matumizi ya teknolojia mpya ikiwemo matumizi sahihi ya
mbolea, mbegu zenye ubora, uboreshaji wa nyanda za malisho na utoaji wa
huduma za ugani na mafunzo kupitia shamba darasa.
Hivyo
kutokana na mukhtadha huu juhudi hizi zote zina lengo la urejesha ardhi
iliyoharibika ili iweze kuendelea kuzalisha mazao ya kilimo, mifugo na
misitu hapa nchini.
Mratibu
wa mradi kutoka Ofisi hiyo, Joseph Kihaule anasema kuwa mradi huo
unajumuisha uanzishwaji wa mashamba darasa 100 katika wilaya hizo
Tanzania Bara na Zanzibar.
Wawezeshaji
wa mradi huo ni Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO), Chuo cha
Kilimo cha Sokoine (SUA) na Wakala wa Taifa wa Mbegu za Miti Tanzania
(TTSA) huku washiriki wa mafunzo wakitoka taasisi mbalimbali za
Serikali.
Miongoni
mwa taasisi hizo ni pamoja na Wizara za Kilimo, Maliasili na Utalii,
Maji, Mifugo na Uvuvi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Ofisi ya Makamu wa Pili
wa Rais Zanzibar Idara ya Mazingira, Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo
na Uvuvi Zanzibar.
Wengine
ni kutoka katika Halmashauri zinazotekeleza mradi huo huku mikoa ikiwa
kwenye mabano ni Mkalama (Singida), Micheweni (Pemba), Magu (Mwanza),
Nzega (Tabora) na Kondoa (Dodoma).
Mradi
huu umenufaisha Watanzania kwa kupanga mipango ya matumizi bora ya ardhi
iliyoandaliwa ambayo itawasaidia kuwa na usimamizi bora wa maliasili,
matumzi endelevu ya ardhi na kupungua kwa migogoro ya matumzi ya ardhi
na maliasili.
Aidha,
mradi huu umewezesha wananchi kupatiwa mikopo kwenye taasisi za fedha,
kuandaa mafunzo kuhusu upangaji wa matumizi ya ardhi yamewajengea uwezo
wa upangaji na usimamizi wa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao.
Pamoja
na hayo pia mradi umesaidia katika uboreshaji wa hali za maisha ya
wananchi kwa matumizi ya taarifa za awali za utafiti lakini pia
wataalamu wamejengewa uwezo wa uanzishaji na uendeshaji wa mashamba
darasa.
Kazi zilizofanyika hadi sasa katika utekelezaji wa mradi Miongoni
mwa kazi zilizofanyika ni kuundwa kwa Kamati za usimamizi wa Maliasili
na Mazingira, Kamati za Mipango Bora ya Matumizi ya Ardhi za vijjiji
katika vijiji vyote vya mradi isipokuwa wilaya ya Micheweni ambako
Kamati za Mipango Bora ya Matumizi ya Ardhi za shehia hazijaundwa.
Pia
yameendeshwa mafunzo ya upangaji wa matumizi ya ardhi kwa maafisa wa
ngazi ya wilaya na vijiji, wajumbe wa Kamati za Mipango ya Matumizi ya
Ardhi za vijjiji, Halmashauri za Vijiji na baadhi ya wananchi na jumla
ya maafisa na wanavijiji 821 wamepata mafunzo hayo.
Kufanya
Tathmini ya utambuzi wa vyanzo vya maji na teknolojia zitakazotumika
kupata maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu, kilimo na mifugo katika
vijiji vyote vya mradi katika wilaya za Mkalama, Nzega, Magu na Kondoa.
Kuandaa
Mipango ya matumizi bora ya ardhi katika vijiji 15 kwenye wilaya za
Mkalama (vijiji vitano), Nzega (Vijiji vitano), Kondoa (vijiji viwili)
na Magu (vijiji vitatu). Uainishaji wa Vipaumbele vya maeneo na makundi
ya watumiaji raslimali kwa ajili ya urejeshwaji wa uoto wa asili na
hifadhi ya bioanuai umefanyika na kukubalika na wadau katika vijiji
vyote vilivyoandaa mipango ya matumizi ya ardhi.
Muda
wa kutekeleza mradi huu ni kwa kipindi cha miaka mitano (2017-2022) na
gharama ya mradi ni Dola za Marekani millioni 7.156. Mfadhili mkuu ni
Mfuko wa Mazingira Duniani (GEF) kupitia Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo
ya Kilimo (IFAD).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇