Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini imezungumzia upinzani wa Marekani kuhusiana na kutumwa bidhaa za kibinaadamu kama vile madawa, chakula na vifaa vya tiba kwenda Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
Kuhusiana na suala hilo serikali ya Korea Kusini imesema kuwa bado inaendelea na mazungumzo na Marekani. Chanzo kimoja cha Wizara ya Mambo ya Nje ya Korea Kusini ambacho hakikutaka kutaja jina lake kimefichua kwamba, serikali ya Seoul inafanya mawasiliano na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa upande mmoja na Marekani kwa upande wa pili kuhusiana na biashara ya sekta ya bidhaa za kibinaadamu. Kwa mujibu wa ripoti hiyo maafisa wa Korea Kusini kutoka Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ya Viwanda na Wizara ya Fedha, wamefanya safari nchini Marekani na kukutana na viongozi wa Washington kuhusiana na suala hilo.
Shirika la Habari la Korea Kusini la Yonhap limebainisha kwamba serikali ya Iran imewasilisha malalamiko yake kwa balozi wa nchi hiyo mjini Tehran na kumfikishia malalamiko yake kufuatia kuzuiwa usafirishaji wa bidhaa na vifaa tiba vya Korea Kusini kuja nchini hapa. Habari mbalimbali zinaarifu kwamba Marekani ilifuta msamaha wa vikwazo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran tangu mwezi Aprili mwaka huu, ambapo kufuatia hatua hiyo mashirika ya Korea Kusini yamekumbwa na matatizo makubwa ya kutuma bidhaa za vifaa tiba, madawa na bidhaa nyingine za kibinaadamu nchini Iran. Kitendo cha Marekani cha kuzuia kutumwa vifaa na bidhaa za tiba nchini Iran, ni ushahidi wa wazi wa madai potofu ya Wamarekani kuwa hawajazuia vifaa vya kibinaadamu kuingia Iran kutokana na vikwazo vyake vya kidhalimu.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇