Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC)
Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) imenza kusikiliza mashtaka yanayohusiana na jinai zai kivita zilizofanyika nchini Afghanistan.
Katika kikao cha kesi hiyo kilichoanza jana mwendesha mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, Bi Fatou Bensouda alitoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusiana na hatua na vitendo vya wanajeshi wa Marekani, mashirika ya ujasusi ya nchi hiyo na vilevile kundi la Taliban na magenge mengine ya kigaidi katika kipindi chote cha vita vya Afghanistan.
Wakili wa wahanga 82 wa ukatili na jinai za kivita nchini Afghanistan, Fergal Gaynor amesema katika kikao hicho kwamba, wateja wake ni wahanga wa jinai na ukatili uliofanywa na pande kadhaa.
Marekani iliivamia ardhi ya Afghanistan mwaka 2001 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na kurejesha amani nchini humo. Hata hivyo tangu wakati huo Washington imeshindwa kutekeleza ahadi yake, na kinyume chake, hali ya ukosefu wa amani, ugaidi na uzalishaji wa dawa za kulevya vimeongezeka kwa kiwango kikubwa nchini Afghanistan.
Maafisa wa serikali ya Afghanistan na raia wa nchi hiyo wamekuwa wakikosoa uwepo wa majeshi ya kigeni katika ardhi ya nchi hiyo na wanataka majeshi ya Marekani yaondoke nchini humo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇