LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 10, 2019

KUFIKIA MEI 2020, YANGA KUBADILI MFUMO WA UENDESHAJI


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Dk. Mshindo Msola amewaahidi wanachama wa timu hiyo kuwa mpaka kufika Mei mwakani watakuwa wameingia katika mfumo wa uwekezaji kwa njia ya hisa.

Kauli hiyo imekuja baada ya maswali mengi kutoka kwa Wanachama wa Klabu hiyo kutokana na klabu kuwa na malimbikizi makubwa ya madeni na kufikia wachezaji kuandika barua za kuachana na timu hiyo.

Dk. Msola amesema hiyo ilikuwa ni ahadi ya pili kwenye kampeni yake na mchakato wake unaendelea hivyo hadi kufikia mwezi Juni itakuwa imekamilika.

Msola ameongeza kuwa katika mchakato huo watawa washirikisha Wanachama katika kila hatua ili maamuzi yawe ya watu wote.

"Mchakato ukienda sawa mpaka Juni mwakani tutakuwa tumeingia kwenye mfumo wa kisasa wa uendeshaji wa klabu kwa uwekezaji wa hisa. Hii ni ahadi yangu kwa Wanachama wa Yanga," amesema Dk.Msola.

Akizungumzia suala la madeni ya mishahara kwa wachezaji, Msola amesema Madeni waliyoyakuta toka mwezi wa 5 walivyoingia ni pamoja na deni la serikali(TRA,Ardhi)  mil 800, fedha za usajili za wachezaji  kwa miaka miwili nyuma mil 250.

Amesema, madai ya makocha waliokowepo akiwepo Hans Van De Pluijm ni Milion  100, deni la golikipa Rostand mil 60, Donald Ngoma,Obrey Chirwa zaidi ya mil 100.

Mapato ya Yanga toka wameingia kutoka kwa wadhamini ni Bilioni 2.2 wakati matumizi ni bil 4 na  mishahara imekwama kwa sababu ya michezo ya CAF ilianza mapema kuliko ilivyotegemewa kwa hiyo ikaharibu bajeti.

Yanga imekuwa inasuasua katika kulipa mishahara kwa wachezaji na kupelekea kuwa na migomo ya mara kwa mara kaa wachezaji.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages