LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Dec 29, 2019

KATIBU MKUU WA CCM DK. BASHIRU ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA MIKOA NA WILAYA

27 Desemba, 2019
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally (Pichani), ametoa maelekezo kwa Wakuu wa Mikoa na  wilaya kuhakikisha wale waliofanya kazi  za ufundi, vibarua, wahudumu na kazi zingine katika miradi mbalimbali ya serikali wanalipwa kwa wakati hasa kwa miradi ambayo serikali tayari ilishatoa fedha hizo.

Dkt Bashiru amesema, kwa wale wasimamizi wa miradi hiyo ambao wamekula fedha na kushindwa kuwalipa wafanya kazi kwa wakati, wakuu wa mikoa na wilaya wasisite kuwachukulia hatua kali za kinidhamu na warudishe fedha hizo ili jasho la wananchi wanyonge lisipotee.

Bashiru ametoa maagizo hayo Desemba 27, 2019 alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Bukoba vijijini, ambapo licha ya kuridhishwa na ujenzi huo lakini amekuwa akipokea malalamiko mbalimbali ya wafanayakazi kutokulipwa kwa wakati licha ya fedha zote shilingi bilioni 1.5 kufikishwa hospitalini hapo.

’’Natoa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya na Mikoa nchi nzima, kuhakikisha wanalinda miradi hii dhidi ya wadokozi na wezi wa rasilimali hizi za wananchi, na wale wote waliotoa jasho lao kujenga miradi hii, yaani mafundi, vibarua, wahudumu na wafanyakazi wengine, walipwe kwa wakati na jasho la mwananchi lisipotee, kama kuna waliohusika katika kuchelewesha malipo yao, wachuliwe hatua kali za kinidhanu kwa mujibu wa sheria za nchi.” Katibu Mkuu amesisitiza.

Aidha, Dkt. Bashiru ametoa wito kwa wenyeviti wote wa vijiji na mitaa nchi nzima kutoa ardhi kwa shughuli za jamii ikiwemo ujenzi wa Hospitali, Shule, Ofisi za umma, n.k kama ambavyo imefanyika katika kijiji cha Kanazi kwa wananchi kujitolea eneo ambalo ujenzi wa hospitali hiyo ya Halmashuri unaendele, ambapo imesaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za ujenzi wa mradi huo.

wakati huo huo, Dkt Bashiru ametumia fursa hiyo kuwataka wanachi kuendelea kuiamini CCM na serikali yake chini ya Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM, ambapo ameweza kudhibiti nidhamu katika serikali na Chama, na mafanikio yanayopatikana sasa ya ujenzi wa hospitali nchi nzima, vituo vya afya, zahanati, barabara, madaraja, umeme, miradi ya maji n.k ni matokeo ya jitihada hizo.

Ziara hiyo imejumuisha viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM wa wilaya Ndg. Evarist Babyegaya na Mkuu wa wilaya Ndg.  Deodatus Kinawiro

Katibu Mkuu yupo nyumbani kwake, Kagera wilayani Bukoba kwa mapumziko ya siku kumi, ambapo anatarajiwa kumaliza mapumziko hayo mwanzoni mwa mwezi Januari, 2020.

Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages