Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally leo tarehe 07 Desemba, 2019 ameanza ziara ya siku mbili wilayani Nzega.
Akiwa katika wilaya hiyo, ametembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ukiwemo mradi wa Shule ya wanawake Mwanzoli ambapo ameridhishwa na maendeleo mazuri ya ujenzi wa shule hiyo na kusisitiza umuhimu wa elimu,
"Nawapongeza sana wananzega kwa kazi hii kubwa, kwa kuwa katika safari ya kujenga letu, ujenzi wa taifa unahitaji taasisi madhubuti, moja ya taasisi hizo ni shule, bila kuwa na shule hakuna heshima, na bila kuwa na heshima hakuna taifa, shule ni kitovu cha utaifa wetu na ndio kitovu cha utu wetu".
Pia wakati akiendelea na ziara yake, amejionea adha ya barabara inayoelekea katika shule hiyo, ambapo katika kipindi cha mvua imekuwa na changamoto kubwa na kutoa maelekezo kwa Wakala wa barabara mijini na vijijini (TARURA) kuhakiksha wanaiweka kwenye mpango barabara hiyo ili kupunguza adha kwa wazazi na wanafunzi.
Aidha, Dkt. Bashiru amekagua ujenzi wa daraja la Nhobola ambalo kipindi cha mvua lilikuwa likikata mawasiliano kati ya kijiji cha Mbogwe na Wela ambalo linatarajiwa kukamilika mapema Aprili, 2020.
Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu amefungua shina la wakereketwa la mawakala wa mabasi stendi ya Nzega.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu ameambatana na viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Bi. Munde Tambwe na Naibu Waziri wa Kilimo na Mbunge wa Nzega (M) Ndg. Hussein Bashe.
Ziara hii ni mfululizo wa kutekeleza maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, viongozi kufanya ziara za kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kuimarisha uhai wa chama.
Imetolewa na;
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Your Ad Spot
Dec 8, 2019
KATIBU MKUU WA CCM DK. BASHIRU AANZA ZIARA YA SIKU MBILI WILAYANI NZEGA.
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇