Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia
watuhumiwa kumi na mbili [12] kutokana na tuhuma za kupatikana na dawa za
kulevya [bhangi], pombe haramu ya moshi [gongo], mali za wizi na pombe kali
zilizopigwa marufuku nchini. Watuhumiwa wamekamatwa katika misako na doria
zinazoendelea hapa Mkoani Mbeya katika kipindi hiki cha kuelekea mwisho wa
mwaka.
KUPATIKANA NA BHANGI.
Mnamo tarehe
27.12.2019 majira ya saa 15:00
Alasiri huko Kijiji cha Shigamba, Kata ya Utengule - Usongwe, Tarafa ya
Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi waliwakamata 1. SAKA JAKOBO [20] 2. GODIUSI NAZARETY [23] 3. ERASTO YOHANA MWAMPAMBA [25] na 4. DENISI EDWARD [22] wote wakazi wa
Shigamba wakiwa na bhangi gramu 35.
Watuhumiwa ni watumiaji na wauzaji wa bhangi.
KUPATIKANA SARE ZA JESHI LA WANANCHI TANZANIA
[JWTZ].
Mnamo tarehe
27.12.2019 majira ya saa 15:00
Alasiri huko Kijiji cha Shigamba, Kata ya Utengule - Usongwe, Tarafa ya
Usongwe, Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata ISAKA JAKOBO [20] mkazi wa shigamba
akiwa na sare za Jeshi la Wananchi Tanzania [JWTZ] ambazo ni mkanda mmoja, kofia moja rangi ya kijani “crown”
mbili, begi moja la mgongoni, kofia moja rangi nyekundu, nishani mbili na
mkanda mmoja wa “RSM”. Mtuhumiwa pia alikutwa akiwa na pikipiki Na. MC 852 BLE “Boxer” rangi nyeusi
inayodhamiwa kuwa ni mali ya wizi.
KUPATIKANA NA POMBE
HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Mnamo tarehe 28.12.2019 majira ya saa 16:00 jioni huko Mapeleme, Kata ya
Ubaruku, Tarafa ya Rujewa, Wilaya ya Mbarali, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi
walimkamata ESTWITA KILIMA [42]
mkazi wa Mapelema akiwa na pombe haramu ya moshi[gongo] lita 28. Mtuhumiwa ni muuzaj na mtumiaji pombe hiyo.
KUPATIKANA BHANGI.
Mnamo tarehe
29.12.2019 majira ya saa 13:00
mchana huko maeneo ya Kibisi, Kata ya Kyimo, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya
Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata AMBOKILE MWAISABILA [38] mkazi wa Kibisi akiwa na bangi kilogram 12. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa
bhangi.
KUPATIKANA
NA MICHE YA BHANGI.
Mnamo tarehe
29.12.2019 majira ya saa 18:00 jioni
huko mtaa wa DDC – Mbalizi, Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe, Wilaya
ya Mbeya Vijijini, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata GADI CHARLES [19] mkazi wa DDC akiwa na
miche 7 ya bhangi ndani ya shamba
lake la mahindi. Mtuhumiwa ni mtumiaji wa bhangi.
KUPATIKANA NA POMBE ZILIZOKATAZWA NCHINI.
Mnamo tarehe
29.12.2019 majira ya saa 16:30 jioni
huko Kijiji cha Talatala, Kata ya Ipinda, Tarafa ya Ntebela,
Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata ROSTA MWASAMBOGO [31] mkazi wa Talatala akiwa na “Win” boksi mbili na boksi moja “Cafe rhum”
kutoka nchi ya Malawi.
KUPATIKANA
NA MALI IDHANIWAYO YA WIZI.
Mnamo tarehe
29.12.2019 majira ya saa 16:00 jioni
huko mtaa wa Mapelele - Mbalizi, Kata ya Utengule Usongwe, Tarafa ya Usongwe,
Wilaya ya Mbeya Vijijini, Mkoa Mbeya. Askari Polisi walimkamata EZEKIA MIKISON [40] mkazi wa Mapelele
akiwa na TV “Sundar” inch 19
inayodhamiwa kuwa ni mali ya wizi.
KUPATIKANA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Mnamo tarehe
29.12.2019 majira ya saa 14:45
mchana huko Kitongoji cha Itete - Ndembo, Kata ya Kabula, Tarafa ya
Busokelo, Wilaya ya Rungwe, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata TUNU KIJUMILE [21] mkazi wa Ndembo
akiwa na Pombe haramu ya Moshi [gongo]
lita 3. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji.
KUPATIKANA
NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Mnamo tarehe
29.12.2019 majira ya saa 18:00 jioni
huko Kitongoji cha Majengo - Mapya, Kijiji na Kata ya Lupa, Tarafa ya
Kipembawe, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata ANNA WESTON [40] mkazi wa Lupa akiwa napombe haramu ya moshi [gongo] lita sita
ndani ya nyumba yake. Mtuhumiwa ni muuzaji na mtumiaji wa pombe hiyo.
KUPATIKANA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO].
Mnamo tarehe
28.12.2019 majira ya saa 16:00 jioni
huko maeneo Igogwe, Kata ya Kawetele, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, Mkoa
wa Mbeya. Askari Polisi walimkamata SAMSOM
MWAKYUSA [23] mkazi wa mtaa wa Bagamoyo akiwa na pombe haramu ya moshi
[gongo] lita 17. Mtuhumiwa ni muuzaj na mtumiaji pombe hiyo.
Imetolewa
na;
[ULRICH
O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇