TAARIFA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally (Pichani), usiku wa tarehe 7 Desemba, 2019 ameongoza mamia ya wananzega katika harambee ya kuchangia ujenzi wa jengo la ukumbi wa mikutano wa CCM wilayani Nzega.
Katika Harambee hiyo iliyoandaliwa na Kamati ya siasa ya wilaya, lengo lilikuwa kukusanya milioni 150 lakini kutokana na hamasa kubwa iliyopo miongoni mwa wanaCCM na ilifanikisha kukusanya milioni 164.
Katika harambee hiyo Kamati ya Siasa iliomba ukumbi huo uitwe "Dkt. Bashiru" kutokana na mchango wake mkubwa katika kuimarisha Chama, katika hali isiyo ya kawaida Katibu Mkuu alikataa ombi hilo, na kupendekeza jina la aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU, wa kwanza mwanamke kutoka mkoa wa Tabora marehemu Bibi. Amina Maufi na kutoa wito kuwa,
"Tuwakumbuke viongozi wetu waliojitolea kukijenga na kukipigania chama chetu, na kila mkoa unawaCCM mashuhuri, wengine walishafariki na wengine wapo hai, tujenge utamaduni wa kukumbuka mchango wao, hivyo napendekeza jina la Amina Maufi aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya TANU mwanamke kutoka mkoa huu wa Tabora, alitoa mchango mkubwa katika chama chetu".
Harambee hiyo ni mfululizo wa utaratibu wa WanaCCM kujitolea michango ya hali na mali katika kukiimalisha Chama.
Imetolewa na;
Said Said Nguya
Afisa Habari
Ofisi ya Katibu Mkuu
CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)
Your Ad Spot
Dec 8, 2019
DKT. BASHIRU AVUSHA LENGO LA SH. MILIONI 150 UJENZI WA UKUMBI WILAYANI NZEGA.
Tags
featured#
siasa#
Share This
About Bashir Nkoromo
siasa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇