Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi,
Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumza na
viongozi wa Chama cha Waajiri (ATE) na Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi (TUCTA) walipokutana kwa lengo la kujadili masuala
mbalimbali ya Wafanyakazi na Waajiri, Novemba 2, 2019 Jijini Dodoma.
Sehemu
ya viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA)
wakifuatilia maelezo ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,
Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama (hayupo
pichani) alipokutana nao Bungeni, Jijini Dodoma. Kushoto ni Rais wa
Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya.
Katibu
Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bw.
Andrew Massawe akifafanua jambo wakati wa kikao hicho cha Utatu
kilichowakutanisha kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali ya
Wafanyakazi na Waajiri.
Baadhi
ya wajumbe kutoka Chama cha Waajiri (ATE) na Ofisi ya Waziri Mkuu
wakifuatilia majadiliano wakati wa mkutano huo uliofanyika Jijini
Dodoma.
Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) Bw. Tumaini Nyamhokya akieleza jambo wakati wa mkutano huo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipitia taarifa wakati wa mkutano na
viongozi wa Chama cha Waajiri (ATE) na Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi (TUCTA) walipokutana kwa lengo la kujadili masuala
mbalimbali ya Wafanyakazi na Waajiri, Jijini Dodoma.
Mkuu
wa Huduma za Kisheria kutoka Chama cha Waajiri (ATE) Bi. Suzan Ndomba
akichangia mada wakati wa mkutano huo uliofanyika Jijini Dodoma. Kulia
ni Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na Wenye
Ulemavu Bw. Andrew Massawe.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇