Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (wa tatu kushoto), akifurahi mara baada ya kufunua pazia kuzindua mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kwenye Hoteli ya Coral Beach, Dar es Salaam Mwishoni mwa wiki. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo wa wizara hiyo, Yusufu Singo na Rais wa Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka na kutoka kulia ni Woinde Shisael Meneja Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42. Mashindano hayo yatafanyika Machi Mosi mwakani.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison
Mwakyembe (wa tatu kushoto), akifunua pazia ikiwa ni ishara ya kuzindua
mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kwenye Hoteli ya Coral Beach, Dar es Salaam
mwishoni mwa wiki. Wanaoshudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Michezo wa
wizara hiyo, Yusufu Singo na Rais wa Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka na
kutoka kulia niWoinde Shisael Meneja
Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon na Pamela Kikulu
Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison
Mwakyembe (kushoto), akikabidhiwa zawadi na Pamela Kikulu Meneja Bia ya Kilimanjaro
Wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42.
Meneja wa Grand Malt, David Tarimo wadhamini wa mbio za Km
5, akielezea kuhusu udhamini huo pamoja na sifa za kinywaji hicho.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo
Woinde Shisael Meneja Mawasiliano wa Kamouni ya Tigo Wadhamini wa Kili Half Marathon akielezea kuhusu udhamini wao na kuwaomba watanzania kuisapoti kampuni hiyo kwa kujisajili kwa wingi kujiunga na mtandao huo mkubwa nchini.
Pamela Kikuli Meneja Bia ya Kilimanjaro Wadhamini wakuu wa
mbio ndefu za Km 42. zielezea kuhusu udhamini wa mbio ndefu na kuitangaza bia
ya Kilimanjaro yenye jina linalotukuza Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio
kikubwa cha utalii nchini.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Executive Solutions Waratibu wa
mashindano hayo, Aggrey Marealle akiongoza hafla hiyo ya uzinduzi na kuelezea umuhimu wa watu
kuanza kujisajili ili kushiriki mashindano
hayo makubwa nchini na nje ya Nchi.
KATIBU MKUU WA TOC, FILBERT bAYI AKIELEZEA UMUHIMU WA WATANZANIA KUSHIRIKI NA KUSHINDA MASHINDANO HAYO, ILI WAPATE FURSA YA KUSHIRIKI MASHINDANO YA OLIMPIKI.
Rais wa RT, Anthony Mtaka akitangaza nyongeza ya bonasi kwa wanariadha watanzania watakaoshinda mashindano hayo.
Waziri Dk. Mwakyembe akihutubia katika hafla hiyo
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leodger Tenga akitoa neno la shukrani wakati wa hafla hiyo.
Waziri Dk. Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa RT, BMT na wadhamini wa mashindano hayo
Waziri Dk. Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa RT, BMT na wadhamini wa pamoja na waandaji na waratibu wa Kilimanjaro Marathoni.
Na
Richard Mwaikenda
WANARIADHA
wa Tanzania
watakaoshinda mashindano ya Kimataifa ya Kilimanjaro Marathon 2020, kuibuka na
kitita cha sh. mil. 7 ambapo sh. Mil 4 ni zawadi ya kawaida na sh. mil 3 ni
motisha.
Motisha
hiyo ilitangazwa na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Antony Mtaka wakati wa hafla ya uzinduzi wa mashindano
hayo, uliofanywa na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe katika Hotel ya Coral
Beach, Masaki, Dar es Salaam jana.
Waziri
Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo, alisema kuwa motisha
hiyo iwe ni kichocheo kikubwa kwa wanariadha wa Tanzania kushiriki kwa wingi na
kushinda mbio hizo.
Alisema
kuwa huwa inashangaza kuona zawadi ya 1-39 zinakwenda kwa wakimbiaji wa kutoka nje, wakati Tanzania ina watu wenye misuli, mikono na vifua lakini
hushindwa, wakati watu hao hao
wakikimbizwa na polisi hukimbia sana.
“Nitafurahi
sana kuona bahasha nyingi za zawadi zikibaki nchini, naomba wenye uwezo mkubwa tushiriki kwenye mbio hizi zenye jina kubwa
kimataifa,” alisema Dk.Mwakyembe.
Aliwapongeza
waandaji wa mashindano hayo ambayo sasa yamekuwa yanavutia watu wengi kutoka
mataifa 56 Ulimwenguni, hali inayochangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Alisema
kitendo hicho kimesaidia sana
kuutangaza Mlima Kilimanjaro na vivutio vingine vya utalii vilivyopo nchini.
Pia imesaidia mashindano hayo kuwa na
wadhamini wengi.
Rais
wa RT, Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa
wa Simiyu, aliwaasa wanariadha wa Tanzania kuachana na kasumba ya kukimbilia
kushiriki mashindano ya nje ambako hata zawadi wanazopewa ni sawa na
zinazotolewa na Kilimanjaro marathoni na
mara nyingine kuzidi.
Aliwataka
wajenge tabia ya kupenda kushiriki mashindano ya nyumbani na hasa Kilimanjaro Marathon yenye hadhi
kubwa sawa na mengine ya kimataifa. Alisema kuwa waandaji wameamua kutoa
motisha ili wanariadha wa kitanzania washiriki kwa wingi na kushinda.
Alisema
kuwa wanariadha wakienda nje kushiriki baadhi hulipwa dola 1000 ambayo ni sawa
na sh. 2,460,000 za Tanzania na wengine hulipwa dola 500, kiasi ambacho ni
kidogo ukilinganisha na zawadi ya sh. mil. 4 na nyongeza ya motisha sh. mil. 3, jumla sh. mil 7 kwa mshindi wa
mbio za Km 42.
Mshindi
wa Tigo Kili Half Marathon Km 21, hulipwa sh. mil. 2 kwa upande wa wanaume na
wanawake pia.Mashindano hayo mwaka huu yametimiza miaka 18 tangu ilipoanzishwa
2001.
Naye, Katibu Mkuu wa Kamati ya Olympic Tanzania TOC, Filbert Bayi, alisema kuwa wanariadha
inabidi wayathamini mashindano ya Kilimanjaro Marathon, kwani ni kipimo tosha
cha washindi kupata fursa ya kushiriki mashindano ya Olympic Tokyo, Japan 2020.
Mwenyekiti
wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT), Leodger Tenga, alisema hakuna njia ya
mkato katika mafanikio, hivyo kuwataka wanariadha kutobweteka, bali wajitahidi
sana kufanya mazoezi ambayo ni msingi wa mafanikio ya ushindi.
Hafla hiyo iliwakilishwa pia na Pamela
Kikuli Meneja wa Bia ya Kilimanjaro wadhamini wakuu wa mbio ndefu za Km 42,
Woinde Chisael Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Simu ya Tigo inayodhamini mbio
za Km. 21 na David Tarimo Meneja wa kinywaji aina ya Grand Malt wadhamini wa mbio
za Km. 5.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇