Balozi
wa China nchini Tanzania, Wang Ke akizungumza wakati wa kutoa tuzo kwa
wanafunzi ambao wanasoma Lugha ya Kichina pamoja na kozi ya Kichina hapa
nchini.Hafla fupi ya kutoa tuzo hizo imefanyika katika ubalozi wa China
jijini Dar es Salaam.
Naibu
waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Wiiliam Ole Nasha akizungumza
wakati wa kutoa tuzo kwa wanafunzi wanaosoma Kichina hapa nchini pamoja
na kozi za kichina. Tuzo hizo zimetolewa jijini Dar es Salaa katika
Ubalozi wa china hapa nchini.
Mmoja
ya wanafunzi walioshindana katika shindano la ubunifu lililofanyika
nchini China na kuiuka kidedea katika kuendeleza Teknolojia ya ulishaji
wa Samaki, Amos Benjamini akizungumza wakati wa kupewa tuzo kwa wanafunzi wanaosoma Somo la kichina na Kozi ya kichinz
Mwanafunzi
kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Gloria Gabriel akizungumza lugha
tatu tofauti ili kuwapa uelewa baadhi ya wachina na watanzania waliofika
katika hafla fupi ya kuwapa tuzo wanafunzi wanaofanya vizuri katika
masomo ya kichina hapa nchuni.
Baadhi ya washiriki.
Wageni Waalikwa.
Naibu
waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Wiiliam Ole Nasha akitoa tuzo
kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali wanaofanya vizuri katika masomo ya
kichina hapa nchini.
Balozi
wa China nchini Tanzania, Wang Ke akitoa tunzo kwa wanafunzi wa vyuo
mbalimbali hapa nchini kwa kufanya vizuri katika masomo ya kichina,
katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam katika ubalozi wa China.
Picha ya Pamoja.
Balozi
wa China hapa nchini, Wang Ke akiteta jambo na Naibu waziri wa Elimu
Sayansi na Teknolojia, Ole nasha wakati wa utoaji tuzo kwa wanafunzi
wanaosoma kichina na kozi za kichina waliopata tuzo bora na tuzo za h
Mwanafunzi
wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Doris Onesmo akiwa na tuzo yake mara baada ya
kutunukiwa jijini Dar es Salaam katika ubalozi wa china.
KATIKA kuendeleza ushirikiano wa seikali ya china na Tanzania nchinya china imekuwa
miongoni mwa nchi inayotoa ufadhili kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa
Tanzania wanaoomba ufadhili wa kusomea kozi mbalimbali nchini china.
Akizungumza
na wakati wa kutoa tuzo ya Balozi , Balozi wa China nchini Tanzania,
Wang Ke kwa wanafunzi wanaosoma Lugha ya kichina hapa nchini katika
vyuo mbalimbali, amesema kuwa ushirikiano baina ya China na Tanzania
unazidi kuimarika zaidi hasa wanafunzi wa Tanzania wanapojifunza Lugha
ya Kichina.
"Kwa
mwaka huu Serikali ya China limetoa nafasi 302 za ufadhili kwa wanafunzi
wanaojifunza kozi mbalimbali nchini". Amesema Wang Ke.
Amesema kuwa Serikali ya China imekuwa nchi inayotoa idadi kubwa zaidi ya nafasi za Ufadhili kwa wanafunzi wa Tanzania.
"Mpaka
sasa wanafunzi 1900 wamepata ufadhili wa serikali ya China na kwenda
kusoma nchini China miongoni mwao wamehitimu nchini china na wamerudi
Tanzania kwaajili ya ujenzi wa sekta mbalimbali hapa nchini". Amesema
Wang Ke.
Hata
hivyo mmoja wa wanafunzi waliopata ufadhili wa China Amos Benjamini
alishiriki katika kambi ya ugunduzi kwa vijana duniani(UNLEASH)
yaliyofanyika Shenzhen aliibuka kidedea kwa kubuni teknolojia ya
kulisha Samaki.
Katika
tuzo hizo wanafunzi 20 wamepata tunzo bora na wengine 60 wamepata tuzo
ya Mafanikio, wanafunzi hao ni kutoka vyuo mbalimbali.
Hata
hivyo Naibu waziri wa Elimu na Teknolojia, Ole Nasha amesema kuwa
ushirikiano wa China na Tanzania haujaanza sasa ushirikiano huu ni wa
mda mrefu hasa ukiona Reli ya TAZARA unaweza ukajua ni wa muda gani.
"Kumekuwa
na vijana wengi sana ambao wanasoma kwenye vyuo mbalimbali kwa msaada
wa serikali ya nchini china kwahiyo China imekuwa sehemu ya wanafunzi wa
kitanzania kwenda kujipatia mafunzo mbalimbali".
Nasha amebainisha kuwa kwa kwa miaka mitatu kunawanafunzi zaidi 200 wameenda kusoma kwa msaada wa china.
Nasha
amesema kuwa ni fursa kwa wanafunzi wa Tanzania kujua Lugha ya kichina
ili waweze kufundisha wanafunzi wengine hapa nchini.
Miongoni
mwa waliopata tuzo bora na tuzo za mafanikio wamesema kuwa Lugha ya
kichina kwa sasa ipo sokoni kwa mtanzania kujua Lugha mbalkmbali duniani
zitamsaidia kupata Ajira hata kwenye makampuni ambayo yanatoa ajira kwa
kuzingatia kigezo cha kujua Lugha yao.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇