Wakimbizi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, wameahidi kurejea makwao iwapo maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo yatarejea katika hali ya utulivu.
Hayo yamejiri baada ya ya kufanyika mazungumzo kati ya marais FĂ©lix Tshisekedi wa Kongo DR na mwenzake Yoweri Museven wa Uganda mjini Kampala, ambapo pande mbili zilifikia makubaliano ya kuwamaliza waasi katika maeneo ya mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kadhalika marais hao wamekubaliana kuinua kiwango cha ushirikiano wa kibiashara sambamba na kukabiliana na maradhi hatari ya Ebola.
Jiunge na mwandishi wa mjini Kampala, Kigozi Ismail kwa taarifa kamili……bonyeza alama ya sauti pale juu……../
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇