Afisa Mkuu wa Wateja Binafsi na Biashara Ndogo na za Kati wa benki ya NMB - Filbert Mponzi akimkabidhi Khalifa Kimaro-mmoja wa mawakala cheti cha ushiriki mafunzo ya uwakala.
Mmoja wa mawakala akiuliza swali kwa watoa mada
Meneja
wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd akimkabidhi Betty
Rutihanda-mmoja wa mawakala cheti cha ushiriki mafunzo ya uwakala.
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawakala – James Manyama akitoa mada
**********************************
MAWAKALA
wa Benki ya NMB Halimashauri za Ubungo na Kinondoni jijini Dar es
Salaam wamepigwa msasa katika Semina ya kuwajengea uwezo na kuboresha
huduma inayomfikia mteja wa NMB katika maeneo yao pamoja na kujilinda na
uhalifu na utakatishaji fedha.
Katika
semina iliendeshwa hivi karibuni katika maeneo ya Sinza na Ilala jijini
Dar es Salaam,Mawakala wa Benki ya NMB walipata fursa ya kupewa elimu
juu ya kumpatia mteja huduma bora, kuuliza maswali na elimu juu ya
kujikinga na vitendo vya kihalifu ikiwemo kupitisha fedha chafu, ambapo
ni kinyume na sheria za nchi.
Akizungumza
katika Semina hiyo Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd,
alisema NMB Wakala ni njia inayomfikishia huduma mteja kwa urahisi zaidi
na kwa wakati.
“Kwa
nini tunawatumia mawakala, tumeona kwamba ni njia moja wapo inayoweza
kutufanya tuwafikie wateja wetu ambao ni watanzania zaidi ya Milioni 60,
hatuwezi kufika kila eneo huwa kidogo kuna ugumu wake lakini kupitia
mawakala tunaweza kuwapata kila eneo wenye uwezo wa kuwahudumia wateja
wetu kama vile ambavyo tumekusudia.
“Mteja
wetu anaweza kutoa pesa, kuweka pesa, ataweza kulipia miamala mbali
mbali, kama kulipia malipo ya maji, umeme, malipo ya serikali na ada za
shule, tunasisitiza kwamba wateja wetu waendelee kutuamini kupitia
mawakala wetu ambao wanaendelea kutoa huduma.
“Tumekuwa
na semina mbali mbali, tukiwa tunaendelea kuwajengea uwezo mawakala ili
waendelee kutoa huduma zetu kwa ukaribu Zaidi. Muhimu ni muongozo wetu
kila mwaka tunataka tuwasikilize changamoto juu ya huduma zetu,
tuwaulize maswali watuulize maswali wote kwa pamoja tuweze kuhakikisha
huyu mtanzania anapata huduma zetu kokote kule anakopatikana kwa ufanisi
mkubwa.
Badru
alisema, sio kwa Dar es Salaam tu, bali wameendesha semina kama kwa
zaidi ya maeneo 40 nchi nzima. Semina hizi zimeleta mafanikio makubwa
sana, hasa kwa kuokoa muda wa mteja, kupata huduma ya uhakika na kwa
urahisi.
“Sisi
kwetu wateja ni wafalme na ndio maana tunaendelea kuwa na huduma za
mbadala kama, wakala, masine za ATM, na NMB Mkononi ili kuweza kumfikia
mteja wetu kiurahisi zaidi.”alisema Badru.
Naye
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mawakala – James Manyama, alisema lengo la
kukutana na Mawakala ni kuwapa muelekeo wa wapi Benki inaelekea kwa
wakati na kuwapa mafunzo jinsi ya kujilinda na utakatishaji fedha pamoja
na kuingiza fedha katika mikono ya gaidi.
“Kama
Mawakala, tunawapa wajibu wa kutunza amana za wateja, kutunza usiri wa
wateja, mawakala wetu wamethibitisha ubora wa huduma zetu na wameahidi
kwenda kutoa huduma bora kwa wateja wetu” alisema Manyama.
Kwa
upande wa Mawakala waliohudhuria semina hiyo walitoa kongole zao kwa
NMB kwa jinsi ambavyo inawajali kwa kuwapaa elimu na fursa ya kutoa
changamoto zao ili kuweza kuboresha huduma zao.
“Nafurahi
sana kuwa karibu na NMB, nafurahia kuwepo katika hii semina, NMB
wanatoa huduma nzuri, pia wako karibu na sisi mawakala wao, kila wakala
anafanya kazi kwa ukaribu sana na tawi lake la NMB linalomhudumia,
nashauri Watanzania wenzagu kuchangamkia fursa ya Uwakala wa NMB maana
inalipa” Tedy Michael – Wakala NMB Makumbusho.
“Tunashukuru
kwa semina hii ambayo imetupa elimu juu ya nini cha kufanya kwa wateja
wetu, tumepata mbinu mbadala ya kutoa huduma bora kwa wananchi na
tunawaahidi benki yetu pendwa ya NMB kuwa tutafanya kazi kwa weledi na
kuhakisha wateja wanafurahia huduma zetu.” Alisema Khanifa Kimaro –
Wakala NMB Kimara.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇