LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 21, 2019

TRENI YA ABIRIA DAR ES SALAAM - MOSHI KUANZA DESEMBA

Abiria wa Kanda ya Kaskazini kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka 2019, abiria wa Kaskazini watakuwa na kicheko kwao baada ya  treni ya abiria kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi kuanza Disemba.

Tayari Shirika la Reli Tanzania (TRC) limetoa tangazo la kuanza kwa usafiri huo na kuthibitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isaac Kamwele.

Waziri Kamwele amesema kama Serikali imefurahi kufikia hatua hiyo ukizingatia treni hiyo ilikuwa ianze tangu Septemba 2019.

Hata hivyo, amesema  kutokana na changamoto za kunyesha mvua na kusababisha baadhi ya miundombinu ikiwemo ya reli kuharibika katika ukanda huo wa Kaskazini ndio maana kukawepo na uchelewaji wa kuanza kwake.

“Sasa ile tabia ya wafanyabiashara pale stendi ya ubungo kulangua abiria tiketi wakati watu wakienda kula sikukuu na ndugu zao itakoma, kwani hata mimi ilishanikuta na kama Serikali tulikuwa tunahangaika kutafuta njia ya kukomesha vitendo hivyo na ujio wa treni hii ya abiria utasaidia,” amesema

Kuhusu nauli, Waziri Kamwele amesema wameacha ileile iliyokuwa ikitumiwa tangu kusitishwa kwa usafiri huo na ndio maana hawakuitisha hata kikao cha wadau kuhitaji maoni ya nauli.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages