Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI, Dkt. Respicious Boniface akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani), kuhusu mafanikio ya Taasisi hiyo kwa miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano ulifanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa MOI, Dkt. Respicious Boniface akizungumza na Waandishi wa Habari (Pichani), kuhusu mafanikio ya Taasisi hiyo kwa miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano, Mkutano ulifanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari-MAELEZO Jijini Dar es Salaam.
(PICHA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO)
TAASISI ya Tiba ya Mifupa,
Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) katika kipindi cha miaka minne ya
Serikali ya Awamu ya Tano imeokoa kiasi cha Tsh. Bilioni 38.4 zilizotakiwa
kutumika kwa ajili ya kusafirisha wagonjwa 43,200 nje ya nchi kwa ajili ya kupata
huduma za matibabu ya upasuaji wa kibingwa.
Hayo yamebainishwa leo Ijumaa
(Novemba 22, 2019) Jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dkt. Dkt
Respicious Boniface na kuongeza kuwa katika kipindi cha miaka minne ya Utawala
wa Serikali ya Awamu ya Tano, Taasisi hiyo imeendelea kuimarisha na kuboresha
huduma mbalimbali za afya kwa wananchi.
Dkt. Respicious anasema kutokana
na maboresho na kuimarika kwa huduma ya afya, Taasisi ya MOI ndani ya kipindi
cha miaka minne imeweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 43,200 waliofanyiwa upasuaji wa kibingwa na hivyo
kuokoa maisha ya Watanzania wengi na pesa za Serikali ambazo zingetumika
kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.
‘Gharama za matibabu za
wagonjwa hao kwa ndani ya nchi zilikuwa Tsh Bilioni 16.5 na kama wagonjwa hao
wangepelekwa nje ya nchi kwa matibabu, jumla ya Tsh Bilioni 54.9 zingetumika,
na hivyo kuifanya taasisi kuokoa kiasi cha Tsh Bilioni 38.4 ambazo zitatumika
kwa shughuli nyingine za maendeleo’’.
Aliongeza kuwa Taasisi hiyo
katika kipindi cha miaka minne iliyopita imeweza kupokea kiasi cha Tsh. Bilioni
16.5 kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali ikiwemo jengo jipya la MOI
pamoja na ununuzi wa vifaa tiba vya kisasa ambavyo vimeweza kuleta mageuzi na
maboresho ya huduma za afya katika Taasisi hiyo.
Akitolea mfano, Dkt. Respicious
anasema katika fedha hizo zilizotolewa
na Serikali, taasisi hiyo iliweza kuongeza idadi ya vitanda kutoka 150 hadi 350
kwa wagonjwa wa kawaida, na kufanya kutowepo na mgongjwa anayelala chini kwa
sasa, sambamba na kuongeza idadi ya vitanda kwa wagonjwa wanaohitaji uangalizi
maalum kutoka vitanda 8 hadi 18.
Aidha Dkt. Respicious anasema
kuwa pia katika fedha hizo, Taasisi hiyo imeweza kuongeza vyumba vya upasuaji
kutoka vyumba 6 hadi 9, kuongeza vyumba 32 vya wagonjwa binafsi vya daraja la
juu pamoja na kuongeza chumba cha upasuaji kwa mgonjwa bila kulazimika kulala
hospitali.
Kuhusu vifaa Dkt. Respicious
anasema, katika fedha hizo, pia Taasisi ya MOI iliweza kununua mashine mpya za
kutolea dawa za usingizi, mashine za kisasa za Radiolagia zikiwemo MRI,
CT-Scan, Digital X-Ray, CR X-ray, Portable X-ray, Ultra Sound 2, ECHO na ECG,
ununuzi wa mashine mbili mpya za kisasa za vipimo vya maabara.
Akifafanua zaidi, Dkt.
Respicious anasema kutokana na maboresho hayo, Taasisi hiyo ndani ya kipindi
cha miaka mine imeweza kufanya upasuaji kwa wagonjwa 43,200 waliofanyiwa
upasuaji wa kibingwa na hivyo kuokoa maisha ya Watanzania wengi na pesa za
Serikali ambazo zingetumika kupeleka wagonjwa nje ya nchi kwa matibabu.
‘Mbinu hii imesaidia kuongeza
idadi ya wagonjwa wa upasuaji kutoka 400-500 kwa mwezi hadi kufikia 700-900 kwa
mwezi, na idadi ya wagonjwa hao waliofanyiwa upasuaji wa kibingwa ni pamoja na
kubadilisha nyonga (900), kubadilisha magoti (870), upasuaji wa mfupa wa kiuno
(618), watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi (2,070)’’ alisema Dkt.
Respicious.
Aidha Dkt. Respicious anasema
Taasisi ya MOI pia imeanzisha huduma mpya ikiwemo huduma ya upasuaji wa
magoti/mabega kwa njia ya matundu ambapo hadi sasa wagonjwa 800 wamefanyiwa
upasuaji pamoja na huduma ya upasuaji wa kuondoa vivimbe vya mishipa ya damu
kwenye ubongo ambapo wagonjwa watano pia wamefanyiwa upasuaji huo.
Anaitaja huduma nyingine kuwa
ni pamoja na uanzishwaji wa wodi maalum ya kulazwa na kufanyiwa upasuaji siku
hiyo hiyo, ambapo wagonjwa 355 wamefanyiwa upasuaji na kufanya upasuaji wa uti
wa mgongo kwa kupitia tundu dogo, ambapo hadi sasa wagonjwa 120 wamefanyiwa
upasuaji.
‘Huduma hizi mpya, zimeiwezesha
Taasisi kupunguza kwa kiasi kikubwa rufaa za wagonjwa nje ya nchi, ambapo kwa
sasa kwa magonjwa ya Neurosurgies asilimia 95 tunafanya hapa na upasuaji wa
mifupa asilimia 98 tunafanya hapa pia’’ alisema Dkt. Respicious
Kuhusu huduma ya tiba mtandao,
Taasisi hiyo kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto imejenga chumba maalum ambapo madaktari katika sehemu mbalimbali za nchi
watatuma picha za X-ray/CT-Scan zitakazosomwa na madaktari bingwa wa radiolojia
na majibu yatarudishwa kwa daktari aliyeomba kwa muda mfupi.
Aidha katika katika eneo la
mafunzo, Dkt. Respicious anasema katika kipindi cha miaka minne ya Uongozi wa
Rais Dkt. John Magufuli, jumla ya madaktari bingwa 50 wa mifupa wamehitimu
mafunzo, ukilinganisha na madaktari 7 waliohimtimu katika kipindi cha miaka
mine iliyotangulia.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇