Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe.
Jeppe Kofod wakati walipokutana ofisini jijini Dar es Salaam. Mawaziri
hao wapo Dar es Salaam kuhudhuria mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya
Nje wa nchi 29 za Afrika na Nordic unaofanyika nchini.
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Kofod akizungumza na Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John
Kabudi (Mb) wakati walipokutana jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili – Kiingereza
Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe. Jeppe Kofod wakati walipokutana
jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) akiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa
Finland Mhe. Pekka Haavisto walipokutana jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto akifafanua jambo kwa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof.
Palamagamba John Kabudi (Mb) wakati walipokutana jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili – Kiingereza
Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto walipokutana
jijini Dar es Salaam. Tukio hili lilishuhudiwa na Balozi wa Tanzania
katika nchi za Nordic, Mhe. Dkt. Wilbroad Slaa na Naibu Katibu Mkuu
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi
Ramadhan Mwinyi.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) akizungumza na Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe.
Ine Eriksen Soreide walipokutana jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) akimkabidhi zawadi ya kamusi ya Kiswahili – Kiingereza
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen Soreide walipokutana
jijini Dar es Sa
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
John Kabudi (Mb) kwa nyakati tofauti amekutana na kufanya mazungumzo na
Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Denmark, Finaland na Norway ambao
wamekuja nchini kuhudhuria Mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa
nchi za Afrika na Nordic unaofanyika jijini Dar es Salaam.
Viongozi
hao wamezungumzia na kukubaliana kuendelea kuimarisha mahusiano mazuri
ya kirafiki na kihistoria yaliyopo baina ya nchi hizo.
Katika
mazungumzo hayo Prof. Kabudi amezieleza nchi hizo kuhusu msimamo wa
Serikali ya Tanzania katika kujiimarisha kiuchumi kupitia ukusanyaji wa
mapato ya ndani ili iendelee kutoa elimu bure na bora kwa watoto wa
kitanzania, huduma bora za afya kwa watanzania, kuwezesha upatikanaji wa
maji safi na salama kwa wananchi wote na kufikisha huduma za Nishati
kwa watanzania wote hasa wa vijijini.
Amesema
kwamba Tanzania itaendelea kutoa kipaumbele kwa Siasa za maendeleo ili
kuhakikisha azma ya kuwa nchi ya uchumi wa kati na wa viwanda inafikiwa.
“Tanzania
haiangalii Siasa za nguvu, tunaangalia Siasa za kuletea wananchi
maendeleo, na kwa mpango huo tutaendelea kuimarisha ukusanyaji wa mapato
yetu ya ndani na kumfanya kila mtanzania kulipa kodi ili tuendelee
kutoa elimu bure ya msingi na sekondari kwa watoto wa Kitanzania,
kuboresha huduma za afya hadi vijijini, upatikanaji wa maji safi na
salama na kuhakikisha huduma za nishati ya umeme zinawafikia watanzania
wote hadi wa vijijini,” alisema Prof. Kabudi.
Amewahahakishia
mawaziri hapo kuwa Tanzania itaendelea kuheshimu makubaliano ya
Kimataifa hasa katika suala la wakimbizi na kuwafanya watu wanaokuja
kutafuta hifadhi za kisiasa nchini kwetu wana pata hifadhi hizo.
Akizungumza
alipokutana na Prof. Kabudi Waziri wa Mambo ya Nje wa Denmark Mhe.
Jeppe Koffod amemuhakikishia Prof. Kabudi Serikali ya Denmark itaendelea
kuiunga mkono Tanzania katika jitihada zake za kuimarisha huduma za
jamii kama vile utoaji wa elimu bure, huduma za afya na maji salama.
Pia
amesisitiza kwamba wataendelea kuunga mkono mpango wa utoaji wa elimu ya
ufundi nchini na kuwafanya vijana wa kike na wa kiume Nchimbi kushiriki
katika harakati za ujenzi wa taifa lao.
Naye
Waziri wa Mambo ya Nje wa Finland Mhe. Pekka Haavisto ameahidi nchi yake
kuendelea kuisaidia Tanzania katika maeneo ya misitu, utawala bora,
ukusanyaji mapato, haki za binadamu na Tehama.Amesema
Finland pia itaendelea kuisaidia Tanzania kwenye Elimu kwakuwa Elimu
imekuwa na mchango mkubwa na hivyo kutoa viongozi wa baadae.
Naye
Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway Mhe. Ine Eriksen Soreide ameipongeza
Serikali ya Tanzania kwa kazi kubwa inayofanya ya kupambana na rushwa na
ufisadi na hivyo kuongeza imani ya Norway kuwezesha zaidi nchini.
Aidha, ameahidi kuwa nchi yake itaendeleza Ushirikiano wake na Tanzania.
Prof.
Kabudi pia amekutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Msumbiji Mhe. Jose
Pacheco na kujadiliana mambo mbalimbali ikiwemo kuimaraisha mahusiano
baina ya Msumbiji na Tanzania.
Mawaziri
hao wako nchini kuhudhuria mkutano wa 18 wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa
nchi 29 za Afrika na Nordic unaofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇