Mkuu
wa Mkoa wa Arusha - Mrisho Gambo(kushoto) akisalimiana na mmoja wa
wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mrisho Gambo ya jijini Arusha
wakati wa hafla iliyofanyika hivi karibuni ya kukabidhiwa meza na viti vyenye thamani ya sh. mil.10 vilivyotolewa na benki ya NMB . Katikati ni Meneja wa NMB
Kanda ya Kaskazini, Aikansia Muro.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kihaka wilayani Kilolo - Iringa wakiwa wamebeba stuli za maabara muda mfupi baada ya kukabidhiwa
na benki ya NMB.Benki ya NMB ilikabidhi meza na stuli 60 vyote vikiwa na thamani ya shilingi Milioni 10.Wanafunzi wa shule ya Msingi Maduma iliyoko Kata ya Maduma Wilayani Mufindi wakishangilia madawati waliyokabidhiwa na benki ya NMB shuleni kwao.
Mkuu
wa Wilaya ya Rorya, Simon Chacha akiwa ameketi na wanafunzi wa shule
ya msingi Minigo mwanzoni mwa wiki katika moja ya madawati yaliyotolewa na
benki ya
NMB ili kusadia kupunguza uhaba wa madawati shule hapo. Wengine ni
Kaimu Meneja wa Kanda ya Ziwa (Mwenye koti na Tai Nyeusi), Amos Mubusi.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇