MKUU
wa Wilaya ya Ubungo – Kisare Makori, akikata Utepe kuzindua rasmi Tawi
jipya la Benki ya NMB Mbezi Louis wakati wa hafla ya uzinduzi huo
iliyofanyika juzi Mbezi Mwisho jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni
Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd, Mkuu wa Idara ya
Wateja Binafsi wa NMB – Omari Mtiga, Katibu Tawala Wilaya ya Ilala –
James Mkumbo na Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo, Fortunata Shija.
MKUU
wa Wilaya ya Ubungo – Kisare Makori (kushoto) na Mkuu wa Idara ya Wateja
Binafsi wa Benki ya NMB – Omari Mtiga (wa pili kulia) wakifunua
kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi jipya la NMB Mbezi Louis.
Kulia ni Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam – Badru Idd.
Benki
ya NMB imefungua tawi lake jipya jijini Dar es Salaam ikiwa ni
utekelezaji wa mpango wake wa kufikisha huduma za kibenki kwa Watanzania
wengi ili kuchochea ukuaji wa uchumi.
Ufunguzi wa tawi hilo la NMB Mbezi Louis unaifanya benki hiyo kuwa na jumla ya matawi matano ndani ya wilaya ya Ubungo pekee.
Akizungumza
katika hafla ya ufunguzi wa tawi hilo mwishoni mwa wiki, mkuu wa
kitengo cha wateja binafsi wa NMB, Omari Mtiga, alisema uamuzi wa
kufungua tawi hilo umetokana na tafiti mbalimbali zilizoonyesha kuwa
Mbezi Louis ni eneo linalokuwa kwa kasi katika biashara.
“Tumeona
eneo hili linakuwa kwa kasi sana kibiashara lakini wateja wetu bado
wamekuwa wakilazimika kusafiri kilometa 15 wakifuata huduma zetu katika
matawi ya Ubungo, Sinza, Mlimani City na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Sambamba na kauli mbiyo yetu ya: Karibu Yako, tumeona tufungue tawi hapa
hapa,” alisema.
Akifungua
tawi hilo, Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori, alisema upatikanaji
wa huduma za kibenki ni muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa
nchi.
“Ufunguzi
wa tawi hili la NMB utasaidia kukuza idadi ya Watanzania wanaotumia
huduma za kibenki ambao kwa hivi sasa wapo chini ya asilimia 20,”
alisema.
Aliipongeza
NMB kwa kuja na njia za kidijiti za kufikisha huduma zake kwa
Watanzania, akitolea mfano wa huduma inayowezesha watu kufungua akaunti
ya benki hiyo moja kwa moja kwa kutumia simu za mkononi bila kulazimika
kwenda katika tawi lolote la benki.
“Hivi
karibuni, NMB imekuja na huduma inayolenga kuwahudumia waendesha
bodaboda. Hii ni hatua inayostahili pongezi,” alisema Makori.
Tawi la Mbezi Louis linaifanya NMB kuwa na jumla ya matawi 224 nchi nzima
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇