Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba
Kabudi amesema kuwa, ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania ( ATCL),
Bombardier Q400 iliyokuwa iwasili nchini hivi karibuni, inashikiliwa
nchini Canada na kesi ipo mahakamani.
Akizungumza
jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuwaapisha Mabalozi mbalimbali, Waziri
Kabudi amesema kuwa, ndege hiyo inashikiliwa baada ya kufunguliwa kwa
kesi mpya, kesi ambayo imefunguliwa na Mkulima aliyeshindwa Kesi
aliyoifungua nchini Afrika Kusini.
Profesa
Kabudi ameongeza kuwa, Serikali imekasirishwa na vitendo vya ndege
zake kushikiliwa nchini Canada, na kwamba tayari amekutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Canada hapa nchini kumueleza kuhusu jambo hilo.
Waziri
Kabudi pia ametumia hafla hiyo kuwataka Mabalozi hao wanaokwenda
kuiwakilisha Tanzania kwenye Mataifa mbalimbali, kwenda kusimamia vizuri
matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali, kwa kuwa kumekua na
matumizi mabaya ya fedha kwenye Ofisi za Ubalozi.
Ametolea
mfano Ubalozi wa Tanzania huko Addis Ababa - Ethiopia ambapo kumekua
na ubadhirifu mkubwa na fedha na kuongeza kuwa kwa sasa Taasisi za
Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) inaendelea na uchunguzi.
Katika hafla hiyo, Rais John Magufuli amewaapisha Mabalozi Watano ambao wanakwenda kuiwakilisha Tanzania katika nchi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇