CAG mpya Kichere- kazi yangu ni kulinda kihenge cha mapato ya serikali
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
Mdhibiti
na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) aliyemaliza muda wake
Profesa Mussa Assad amesema kuwa anakwenda kufanya kilimo kutokana na
uwekezaji alioufanya katika siku hivi karibuni baada ya kustaafu nafasi
hiyo watu mjini wakinihitaji nitakuja .
Profesa
Assad ameyasema hayo wakati wa makabidhiano na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu
wa Hesabu za Serikali Mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika
kwenye Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi (NAOT),leo jijini Dar es Salaam.
Profesa
amesema kuwa katika kufanya kazi amewashukuru wafanyakazi wa ofisi hiyo
kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote cha utumishi na kumtaka
CAG mpya afanye ushirikiano nao kwani watu hao wamejengwa kwa muda mrefu
na sifa zote .
Assad
amesema kuwa katika kufanya kazi tumejenga mahusiano na wadau
mbalimbali wa nje ambao ndio watu wa kujengeana uwezo na sio kwa ndani
“Changamoto
ni nyingi tumepitia lakini siwezi kutia ukakasi katika hili na watu
niliowakosea, naomba wanisamehe kwani sisi ni binadamu”amesema Profesa
Assad
Kwa upande wa CAG Charles Kichere mpya amesema kuwa kazi kubwa ni kulinda kihenge anajua kazi ngumu ya ukusanyaji wa mapato.
Kichere
amesema ataifanya kazi hiyo kwa weledi na uadilifu kwa kushirikiana na
timu yake ya ofisi ya Taifa ya mkaguzi ikiwa na kuangalia mapato ya nchi
yanatumikaje kwa kuangalia ripoti sambamba na kujenga timu imara na sio
watu walisambaratika.
Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake Profesa
Mussa Assad akimkabidhi nyaraka za ofisi CAG mpya Charles Kichere katika
hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi
na Mdbiti Mkuu wa Hesabu za Serikali aliyemaliza muda wake Profesa
Mussa Assad akizungumza mara baada ya makabidhiano ya nyaraka na CAG
mpya Charles Kichere katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam.
Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) mpya Charles Kichere
akizungumza mara baada ya kukabidhiwa na aliyekuwa CAG Profesa Mussa
Assad katika hafla iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkaguzi
na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG) Mpya Charles Kichere akiwa na maua
mara baada ya kupokewa wakati akiwasili katika ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi kwa ajili ya makabidhiano ya Ofisi ya aliyekuwa CAG Profesa
Assad jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇