Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akimsikiliza Mkurugenzi wa
Uwekezaji na Miradi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es
Salaam (DAWASA), Mhandisi Ramadhani Mtindasi katika kituo cha kusukumia
maji Kibamba, wilayani Ubungo.

Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) pamoja na Mkuu wa Wilaya za
Ubungo, Kisare Makori (kulia) na Mkuu Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo
(kushoto) katika ziara ya kufuatilia utekelezaji wa Mradi wa Maji wa
Kisarawe, katika Kata ya Kibamba, wilayani Ubungo.

Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa na mkandarasi alipotaka
maelezo kuhusu utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa kwake jana ya
kukamilisha utaratibu wa malipo na kazi ya kuvuta umeme.

Tenki
la maji la Kibamba lenye ujazo wa lita milioni kumi litakolotumika
kuhifadhi maji yatakayo hudumia wakazi wa Kisarawe kupitia Mradi wa Maji
wa Kisarawe.

Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa na Msimamizi wa Ujenzi wa
Mradi wa Maji wa Kisarawe, Mhandisi Ishmaeli Kakwezi wakati akikagua
tenki la maji la Kibamba lenye ujazo wa lita milioni 10.

Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa kwenye eneo palipo na
maunganisho ya bomba la tenki la Kibamba na bomba linalopeleka maji
katika Mji wa Kisarawe.
…………………….
Naibu
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) ametembelea na kukagua
utekelezaji wa kazi ndogo zilizobaki katika ujenzi wa Mradi wa Maji wa
Kisarawe katika Kata ya Kibamba, wilayani Ubungo.
Ziara
imelenga kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa jana kwa
mkandarasi kukamilisha utaratibu wa malipo na kazi ya kuvuta umeme
ifanyike haraka ili mradi uanze kufanya kazi mwezi ujao.
Malipo
ya Shilingi milioni nane kwa TANESCO yameshafanyika na kazi ya kufunga
umeme huo itaanza mara moja tayari kwa kufanya majaribio ya kusukuma
maji (pump test) wiki ijayo.
Katika
ziara hiyo Naibu Waziri Aweso ameambatana na Wakuu wa Wilaya za Ubungo,
Kisare Makori na Kisarawe, Jokate Mwegelo akiwasisitiza umoja na
ushirikiano katika kufanikisha zoezi la utekelezaji wa mradi huo kwa
maslahi mapana ya wananchi wa Kisarawe.
Mkuu
wa Wilaya ya Ubungo, Kisare Makori ametoa rai kwa viongozi na watendaji
wa wilaya za Ubungo na Kisarawe kujitoa na kusimamia miradi ya
maendeleo inayotumia fedha nyingi, hatua itakayosaidia juhudi za
Serikali kuzaa matunda.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇