LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 14, 2019

MJUMBE WA UN LIBYA ALIKOSOA BARAZA LA USALAMA KWA KUSHINDWA KUTATUA MGOGORO WA NCHI HIYO

  • Ghassan SalamĂ©
Mkumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya amelikosoa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kuchukua maamuzi kuhusiana na nchi hiyo.
Ghassan Salamé pia amezikosoa nchi kubwa duniani kutokana na misimamo yao kuhusiana na mgogoro wa ndani wa Libya na kuzitaka zisichukue maamuzi kuhusiana na Libya badala ya wananchi wa nchi hiyo.
Ghassan Salamé pia amezitaka nchi wanachama katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuafikiana juu ya mgogoro wa Libya.
Tarehe 4 Aprili mwaka huu wapiganaji wa lile linalojiita jeshi la taifa la Libya linaloongozwa na Khalifa Haftar anayeungwa mkono na kusaidiwa na Saudi Arabia, Imarati, Misri na baadhi ya nchi za Magharibi, walianzisha mashambulizi makali dhidi ya mji mkuu wa nchi hiyo, Tripoli. Takwimu za Umoja wa Mataifa zinasema kuwa, mashambulizi hayo yamesababisha mauaji ya raia wasiopungua 1093 na kuzidisha mgogoro wa ndani wa Libya. Zaidi ya watu wengine laki moja na 20 elfu wamelazimika kuwa wakimbizi.

Wakimbizi wa Libya

Mwezi uliopita wa Oktoba Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) lilitangaza kuwa uhalifu wa kivita na ukiukaji wa haki za binadamu umefanyika katika mapigano ya Tripoli mji mkuu wa Libya na viunga vyake.
Taarifa ya Amnesty International ilisema kuwa, jinai hizo za kivita kwa kiasi kikubwa zilifanywa na wanamgambo wanaoongozwa na kamanda Khalifa Haftar.  

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages