Madaktari wanawake wa chama cha MEWATA wakimsikiliza mgeni rasmi(hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 18 wa chama hicho
Aliyekuwa Rais wa MEWATA miaka ya nyuma Dkt. Merina Njelekela akitoa neno la shukrani
\\Picha ya pamoja ya Mgeni rasmi na wanachama wanaoshiriki mkutano
huo wa mwaka wenye kauli mbiu "Umuhumu wa chanjo ya HPV katika
kukinga saratani ya mlango wa kizazi".
Na. Catherine Sungura-Morogoro
Chama
cha Madaktari Wanawake Tanzania (MEWATA) kimetakiwa kuweka msisitizo
kwenye masuala ya utoaji elimu kuhusiana na chanjo nchini ili idadi ya
watoto wanaopatiwa chanjo kufikiwa.
Hayo
yamesemwa leo na Mkurugenzi wa Tiba kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Grace Magembe wakati wa ufunguzi wa
mkutano wa mwaka wa chama cha Madaktari Wanawake Tanzania ambao
unafanyika mkoani hapa.
Dkt. Magembe amesema
kuwa elimu ya afya kwa wananchi inatakiwa kushushwa hadi chini ili
taarifa kuweza kuwafikia walengwa wengi na hivyo kuweze kufika kwenye
vituo vya afya kupata chanjo ili kuwakinga watoto katika hatari ya
magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.
"Suala la chanjo ni la
kuwekea msisitizo hivyo endapo tutashirikiana katika utoaji wa elimu
hususan pale wizara inapokuwa na kampeni za chanjo ili watoto wetu
wachanjwe na kufikia adhima ya serikali ya kuwa na watoto waliokingwa
kwa chanjo inatimia”.
Hata hivyo amekishukuru
chama hicho kwa kutoa huduma za afya kwa upande wa wanawake hususani
saratani ya mlango wa kizazi na ile ya matiti
“Wanawake
ni taifa kubwa na kauli mbiu ya serikali ya awamu ya tano ni uchumi wa
kati kupitia viwanda hivyo hatuwezi kuwa na uchumi wa kati endapo
wananchi wake ni wagonjwa hususani wanawake ambao ni wazalishaji”
Alisisitiza Dkt. Magembe.
“Serikali inatambua
mchango wengu MEWATA kwa upande wa saratani kwa miaka mingi hivyo
imeweza kujenga vituo vya kutolea huduma zaidi ya mia nne na katika
hivyo asilimia sabini ni vituo vya afya ambavyo vinatoa huduma ya
upasuaji nchini yote inatokana na mchango wenu kwani mlipita nchi nzima
kuwasaidia wanawake licha ya mazingira yaliyokuwepo”.
Hata
hivyo alisema hivi sasa magonjwa yasiyoambukiza yanachangia asilimia
arobaini ya vifo nchini hivyo serikali kupitia wizara ya afya ilifanya
tathimini ya sera ya afya na kuona magonjwa hayo yanaongezeka kwa kasi
na kuua watu wengi na kisababishi kikubwa ni mtindo wa maisha pamoja na
vyakula
“kwa kuona hili kama wizara imekuja
na mpango wa taifa wa magonjwa yasiyoambukizwa ili kila mdau aweze
kuunganisha nguvu katika kupambana na magonjwa haya”.
Aidha,
alibainisha kuwa saratani ya mlango wa kizazi ni kati ya magonjwa
yanayoongoza kusababisha vifo kwa wanawake kwa takribani asilimia
hamsini ya wanawake wote wanaoonwa na saratani ya mlango wa kizazi
inaongoza ikifuatiwa na saratani ya matiti.
Kwa
upande mwingine Mkurugenzi huyo amewata MEWATA kutafuta namna ya
kushughulika na vitendo vya unyanyasaji na ukatili wa kijinsia kwa
watoto wadogo na wanawake kwani vitendo hivyo sasa hivi vimekua
vikiongezeka kila siku,
na hivyo kukitaka
chama hicho kutoa elimu kwa jamii ili kuondoa vitendo hivyo kwa
kuhakikisha inazungumza na jamii kuhusu suala la ukatili kwa watoto
kwani hivi sasa watoto hawako salama na wanaathirika kisaikolojia na
endapo jamii haitashiri katika malezi ya watoto jamii haitokuwa vizuri
miaka ijayo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇