LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Nov 10, 2019

MAGAIDI 25 WA ADF WAANGAMIZWA NA JESHI LA DRC MJINI BENI

Mkuu wa operesheni hiyo, Jacques Ndurua ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, wanajeshi saba wa Kongo DR wameuawa pia katika makabiliano hayo na kundi hilo la kigaidi katika mji wa mashariki wa Beni, ulioko katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Amesema jeshi la nchi hiyo limefanikiwa pia kudhibiti maeneo manne ambayo yalikuwa ngome za wapiganaji hao mkoani Kivu Kaskazini, katika operesheni hiyo iliyoanza tangu Oktoba 30.
Katika miezi ya hivi karibuni, wanamgambo hao wa ADF ambao asili yao ni Uganda wamekuwa wakiwashambulia maafisa wa afya wanaopambana na ugonjwa hatari wa Ebola, mashariki mwa nchi.
Kliniki ya kutibu Ebola iliyoshambulia na waasi
Mwishoni mwa mwezi Mei mwaka huu, jeshi la DRC lilitangaza habari ya kuua wanamgambo wengine 26 wa ADF karibu na mji huo wa Beni ulioathiriwa na ugonjwa hatari wa Ebola, mashariki mwa nchi. 
Juhudi za kupambana na ugonjwa wa Ebola mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo zimeendelea kukabiliwa na vizingiti kutokana na makundi hayo ya wanamgambo kushambulia madaktari na vituo vya afya vinavyotoa matibabu kwa wagonjwa wa maradhi hayo.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages