Na Robertha Makinda, BRELA
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
Bw. Emmanuel Kakwezi amesema kwamba, moja kati ya mafanikio
yaliyopatikana katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya
tano chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph
Pombe Magufuli ni utoaji wa huduma zake zote kwa njia ya mtandao.
Bw.
Kakwezi ameyasema hayo akiwa katika mkutano na Waandishi wa Habari
katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es
Salaam ulioandaliwa na Idara ya Habari Maelezo.
Ameeleza
kwamba Wananchi wanaweza kuwasilisha maombi ya huduma zote zinazotolewa
na BRELA popote pale walipo nchini kwa Mfumo wa Usaili kwa njia ya
mtandao, (Online Registration System / ORS).
Hivi
sasa maombi yote ya Usajili yanatumwa kwa njia ya Mtandao, iwe ni
Usajili wa Kampuni, Usajili wa Jina la Biashara, usajili wa Alama ya
Biashara au Huduma, utoaji wa Leseni za Viwanda, utoaji wa Leseni za
Biashara kundi A na utoaji wa Hataza amesema Bw. Kakwezi.
Bw.
Kakwezi ameongeza kwamba Mabadiliko haya yanaambatana na faida nyingi,
ikiwa ni pamoja na kupunguza muda wa kufanya usajili, mathalani usajili
wa Kampuni hivi sasa unaweza kukamilika ndani ya siku moja. Mfumo huu
uwasaidia watumiaji kutuma maombi yao popote pale walipo nchini nan je
ya nchi vilevile.
Zaidi
ya hilo mfumo huu unamsaidia mtumiaji kufuatilia maendeleo ya maombi
yake na kupata mrejesho kwa ajili ya kufanya marekebisho pale maombi
yanapoonekana kuwa na kasoro.
Aidha
katika kipindi cha miaka minne, BRELA pia imefanikisha uanzishwaji wa
Shahada ya Uzamivu ya Miliki Ubunifu kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam (UDSM), Shirika la Miliki Ubunifu la Kanda (ARIPO) na
Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO).
Mpango
huu una lengo la kuongeza elimu kwa Umma na wataalam katika eneo la
Miliki Ubunifu. Shahada hiyo ya Uzamivu imeanza kutolewa mwezi Agosti
2019.
BRELA
kwa kushirikiana na COSTECH pamoja na Shirika la Miliki Ubunifu Duniani
(WIPO) imetekeleza mradi wa Upatikanaji wa taarifa za teknolojia
zilizopo kwenye kanzidata za Hataza (TISCs) kwa ajili ya kutumiwa na
watafiti na watumiaji wengine ambapo jumla ya Hataza milioni sabini na
sita (76,000,000) zinaweza kupatikana kwenye kanzidata husika.
Katika
kipindi cha Miaka minne, BRELA imefanikisha kuanzisha Utoaji wa Leseni
za Biashara kundi A na kundi B kwa njia ya mtandao. Mfumo huu
umeunganishwa na Mifumo ya Malipo ya Serikali yani Government Electronic
Payment Gateway (GEPG) na Mfumo wa Taarifa za Makusanyo ya Mapato wa
Mamlaka za Serikali za mitaa yaani Local Government Revenue Collection
Information System (LGRCIS).
Majaribio
ya Mfumo huu yalianza tarehe 1 Oktoba 2019 na mpaka sasa Leseni za
Biashara Kundi A zinazotolewa na BRELA na Leseni za Biashara kundi B
katika Manispaa za Bukoba, Chalinze, Wilaya ya Karagwe,Mji wa Mafinga,
Manispaa za Ilala na Halmashauri za Jiji la Mwanza zinatolewa kwa njia
ya Mtandao.
Katika
utoaji wa Leseni kwa mfumo huu takwimu zinaonesha jumla ya Leseni za
Biashara 1206 zimetolewa kupitia mfumo huo ambapo kati ya hizo BRELA
imetoa Leseni 470, Jiji la Mwanza Leseni 199 na Manispaa ya Ilala Leseni
537.
Bw.
Kakwezi ameeleza zaidi kwamba ndani ya miaka minne BRELA imefanikiwa
kuanzisha dirisha la Mfumo wa utoaji wa taarifa za Kibiashara za
Kimataifa. Dirisha hili linamuwezesha mtuamiaji au mwombaji kufahamu
taarifa mbalimbali za upatikanaji wa Leseni na vibali kwa bidhaa
zinazouzwa nje na zinazoingizwa ndani ya nchi.
Dirisha
hili linatoa fursa kwa mwombaji kutembelea tovuti ya
www.trade.business.go.tz na kupata taarifa zote za Biashara
zinazohusiana na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi (Export) na uaigizaji
ndani ya nchi (Import).
Vilevile
mtumiaji atafahamu Sheria, Kanuni, taratibu muda utakaotumika pamoja na
gharama za kila aina ya huduma (Administrative procedures)
atakayohitaji na wapi apite ili kufanikisha upatiakanaji wa huduma
anayohitaji.
Wakala
wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) ilianzishwa chini ya sheria ya
wakala wa serikali namba 30 ya Mwaka 1997 na hatimae kuzinduliwa rasmi
tarehe 3 mwezi Disemba 1999.
BRELA
ipo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara na ilianzishwa kwa ajili ya
kuratibu shughuli za biashara na kudhibiti sheria pamoja na utoaji wa
huduma za Usajili wa Kampuni, usajili wa majina ya biashara, usajili wa
alama za biashara na huduma, utoaji wa leseni za viwanda, utoaji wa
leseni za biashara kundi, utoaji wa Hataza na Miliki bunifu.
Kaimu
Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
Bw.Emmanuel Kakwezi (mbele) akizungumza na waandishi wa Habari leo
katika Mkutano wa BRELA na vyombo mbalimbali vya Habari kuzungumzia
mafanikio ya BRELA ndani ya Miaka minne ya Serikali ya awamu ya tano.
Mkutano huo umeandaliwa na Idara ya Habari maelezo na umefanyika katika
Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC),Jijini Dar
es Salaam.
Baadhi
ya Wanahabari wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye mkutano huo
uliofanyika leo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius
Nyerere (JNICC),Jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇