Mkazi
wa Kijiji ha Bukabile, Specioza Mahondola akitwishwa ndoo ya maji na
Mkuu wa Wilaya ya Busega, Tano Mwera baada ya kupokea mradi kisima cha
maji uliojengwa na taasisi ya The Desk & Chair Foundation
(TDCF).Kushoto anayehushudima ni mwenyekiti wa taasisi hiyo Sibtain
Meghjee.
NA BALTAZAR MASHAKA, BUSEGA
TAASISI
ya The Desk & Chair Foundation imetumia sh.milioni 20 kutatua kero
ya maji iliyodumu kwa miaka 59 ikiwakabili wananchi wa Kijiji cha
Bukabile na Kituo cha Afya Nassa wilayani Busega katika Mkoa wa Simiyu.
Kisima
hicho kirefu cha maji kitatumiwa na wananchi wa kijiji hicho, wakiwemo
wajawazito, wagonjwa wanaotibiwa na kulazwa kwenye kituo hicho cha afya
huku taasisi hiyo ikitoa sh. 800,000 kugharamia vitambulisho vya
wazee 800 vitakavyowatambulisha kupata matibabu.
Mwenyekiti
wa TDFC, Sibtain Meghjee, akikabidhi mradi huo kwa serikali, alisema
kisima hicho kirefu cha maji kimegharimu sh. milioni 20 na kimefungiwa
pampu ya kusukuma maji inayotumia nguvu ya umeme jua na hivyo
kukiwezesha kituo cha Afya Nassa na wananchi kupata maji ya uhakika muda
wote.
“Tumeridhishwa
na mfumo wa mitambo iliyofungwa kisimani hapo kuwa inasukuma maji
vizuri hadi kituoni baada ya majribio kufanyika.Kwa niaba ya wafadhili
na uongozi wa The Desk & Cair Foundation, tunaikabidhi serikali
mradi huu, hatutakuwa na mamlaka nao isipokuwa kwa matengenezo ya
mitambo itakapoharibika,”alisema.
Meghjee
alisema taasisi hiyo imetekeleza miradi mbalimbali ya kijamii mkoani
Simiyu ikiwa ni pamoja na kuboresha visima vifupi 11 vya maji na
kuchimba vipya 12, kufunga mitambo ya umeme jua kwenye Kituo cha Afya
Nassa, mradi wa maji safi na salama Lamadi, baiskeli 5 kwa walemavu wa
viungo na moja ya kawaida.
Mingine
ni mradi wa nyumba 10 za nyasi vijijini kufungiwa mfumo wa umeme
jua,vyoo kwenye shule ya Malayele,vibebeo 300 kwa wajasiriamali na
vitambulisho vya afya kwa wazee 800 huku miradi kama hiyo ikifanyika pia
kwenye mikoa ya Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kati.
“Naishukuru
serikali kwa kutoa vibali na ushirikiano wa dhatiwakati tunapotekeleza
shughuli zetu kwa jamii katika maeneo mbalimbali ya nchi,kama ilivyo
kauli mbiu yetu ya Tupo pamoja Iwe Dhiki Iwe Faraja:Huduma kwa Jamii
Bila Kuchagua Bila Kubagua,”alisema Meghjee.
Aidha,
baadhi ya akinamama wa Kijiji cha Bukabile ambao ni wanufaika wa mradi
huo, Nadhifa Yusuf, Specioza Mahondola naWinfrida Masalu,walisema
utainufaisha jamii na umewakomboa na adha ya kufuata maji umbali
mrefu,ambapo wakati wa kujifungua walipata shida ya kwenda na maji .
Walieleza
kuwa wameteseka miaka mingi kufuata maji umbali wa km 4 kutokana na
kijiji hicho kuwa mbali na Ziwa Victoria, walikuwa wakinunua maji
sh.1000 kwa ndoo tano ama kuyateka kwenye madimbwi hivyo kwa sasa
wataweza kushiriki shughuli za uzalishaji na maendeleo.
Kwa
upande wa vitambulisho vya bima kwa wazee, mmoja wa wanufaika hao Kitula
Kubangwa (71) aliishukuru The Desk & Chair Foundation kuwaondolea
changamoto ya vitambulisho vya matibabu na kuishauri serikali iendelee
kuwatizama kwa jicho la huruma.
Akipokea
mradi huo Mkuu wa Wilaya ya Busega,Tano Mwera, alisema The Desk &
Chair Foundation ni wadau wakubwa wa maendeleo kutokana na misaada yao
kuunga mkono jitihada za serikali katika kuboresha huduma mbalimbali kwa
jamii.
Alisema
mradi huo wa maji utabadilisha maisha ya wananchi na wagonjwa
wanaotibiwa kwenye kituo cha afya Nassa kwani lengo la serikali ni
kumtua mwanamke ndoo ya maji kichwani.
“Maji
ni muhimu, mradi huu unaunga mkono juhudi za serikali za kuhudumia
wananchi na kuwaletea maendeleo lakini pia sasa watayapata maji karibu
na akinamama watatumia muda wao mwingi kufanya shughuli za
maendeleo,”alisema Mwera.
Awali
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nassa, Fred Mruma, alisema changamoto
ya maji tangu kujengwa kwa kituo hicho mwaka 1960 imekwisha ingawa bado
wana tatizo la nishati ya umeme kwenye chumba cha upasuaji, mashine ya
kufua nguo za wagonjwa na mashine ya kupima damu (Full Blood picture
machine).
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇