Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawla za Mkioa na Serikali za
Mitaa, Josephat Kandege (katikati) akiwa ameshikana mikono na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Abdulmajid Nsekela (kushoto kwake) na Mkuu wa
Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri (kulia kwake) pamoja na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (Bot), Benard
Kibese (kulia) na Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa CRDB kukopesha Wajasiriamali wenye vitambulisho vya JPM bila riba wala dhamana. Hafla hiyo ilifanyika jana wilayani Kigamboni, Dar es Salaam. (PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
Mbunge wa Jimbo la Kigamboni, Dk. Faustine Ndugulile (kushoto) akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Nsekela kwa kuanzisha huduma hiyo ya mkopo. Wa pili kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri na Naibu Waziri wa TAMISEMI, Josephat Kandege
pamoja na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (Bot), Benard Kibese (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Nsekela.
Mkurugenzi wa Utafiti wa Masoko na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akifurahia pamoja na Wajasiriamali waliobahatika kupata mkopo usio na riba wala dhamana.
Mgeni Rasmi wa sherehe hiyo, Naibu Waziri wa Tamisemi, Kandege (aliyekaa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Benki ya CRDB, Wilaya ya Kigamboni, Benki Kuu na wadau waliowezesha sherehe hiyo.
Mbunge wa Kigamboni ambaye pia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Dk. Ndugulile akimpongeza Dk. Nsekela kwa huduma hiyo mpya ya mkopo usio na riba kuanzia katika jimbo hilo.
Kandege akiwasalimia Wajasiriamali walihudhuria hsrehe hizo za uzinduzi wa mikopo isiyo na riba kwa wenye vitambulisho vya JPM.
Wakifurahia kupata mikopo hiyo
Viongozi wakiwa na furaha wakati wa hafla hiyo
Baadhi ya Wajasiriamali wakitoa ushuhuda wa kupata mikopo hiyo na kuipongeza CRDB
Mwenyekiti wa Tasisi ya Diligent Conulting Ltd, Profesa Andrew Temu akielezea jinsi wateja watakavyonufaika na mkopo huo kutoka CRDB
Kikundi cha ngoma za asili ya Simba, kikitumbuiza wakati wa hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Nsekela akielezea lengo lao la kuanzisha huduma hiyo ya mikopo isiyo na riba kwa Wajasiriamaliwenye Vitambulisho vya JPM.
Naibu Gavana wa BoT, Dk, Kibese akielezea jinsi benki hiyo ilivyopunguza rkwa mikopo wanayoipzipatia benki jambo liilofanya CRDB iwe ya kwanza mikopo isiyo na riba wala dhamana kwa Wajsiriamali.
Wajasiriamali wakifurahi na kucheza huku wakiimbishwa wimbo na Msanii Zena Mohamed aka Shilole wakati wa hafla hiyo.

Na
Richard Mwaikenda, Kigamboni.
NAIBU
Gavana wa Benki ya Tanzania (BoT), Dk. Benard Kibese na Naibu Waziri Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Josephat Kandege
wameipongeza Benki ya CRDB kuanzisha
Mkopo wa Jiwezeshe usio na riba wala
dhamana kwa Wajasiriamali wenye vitambulisho vilivyotolewa na Rais wa Jamhuri
ya Muungano, John Magufuli.
Pongezi
hizo zilitolewa kwa nyakati tofauti wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mikopo
hiyo kwa Wajasiriamali 3400 wa Wilaya ya Kigamboni, iliyofanyika jana kwenye
ukumbi wa Hoteli ya Kibada Garden, Kigamboni Dar es Salaam.
Dk.
Kibese ameipongeza benki hiyo kwa kuwa ya kwanza kutoa mikopo bila riba kwa wananchi, kitendo
kinachosaidia ukuaji wa uchumi wa Nchi na kipato kwa kila Mtanzania. Mikopo
hiyo hutolewa kwa njia ya simu yaani Akaunti ya Simu (SimAccount).
Naibu
Gavana, ameutaka uongozi wa CRDB kuongeza wigo wa kukopesha kutoka
Wajasiriamali 3400 hadi 10000 kwa Wilaya ya Kigamboni ambayo hadi sasa imeshauza vitambulisho vya
JPM zaidi ya 22,000. Pia alitaka huduma hiyo isambae nchi nzima.
Amezitaka
benki na taasisi zingine za fedha kuiga mfano huo wa CRDB kwa kuanzisha huduma
kama hizo kwa wananchi, hasa kutokana na BoT kupunguza riba kwa mikopo
wanayozipatia benki na taasisi hizo ili nazo zitoe unafuu wa riba kwa wateja
wao.
Pia,
Dk. Kibese alisema kuwa BoT imeamua kutoa sh. bil. 600 za kulipa deni la ndani
kwa wakandarasi, wafanyabiashara ambao nao hulipa madeni kwa wanaowadai
zikiwemo benki ili nazo ziendelea kukopesha.
Naibu
Waziri wa Tamisemi, Kandege, Aliupongeza uongozi wa Benki ya CRDB kwa kuunga
kwa dhati juhudi za Rais John Magufuli za kuwawezesha Wajasiriamali na
kukiongezea thamani kitambulisho cha Wajasiriamali maarufu kama
Kitambulisho cha JPM.
“Mmefanya
kwa dhati kujumuisha vijana na akina mama
katika mikopo, kwani wanashirikiana bega kwa bega na Serikali
kuwawezesha kiuchumi na kuiletea Nchi maendeleo,”alisema Kandege.
Ametaja
baadhi ya faida zinazotokana na uwepo wa Vitambulisho vvya JPM ambavyo hadi sasa vimeuzwa kwa wajasiriamali
mil. 1.8 kwa nchi nzima kuwa ni; kuongezeka kwa wanaotaka huduma, kuwepo mfumo mzuri wa biashara, kuongezeka wigo wa walipa kodi, kuongezeka
wanaojiunga na Bima ya Afya, mifuko ya hifadhi ya jamii, kurasimisha biashara na pato la Taifa, ukusanyaji wa
takwimu muhimu pamoja na kuwaondolea adha na usumbufu Wamachinga.
“Hongera
sana CRDB kwa ubunifu huu wa kutoa mikopo kwa kutumia vitambulisho va JPM, ni
heshima kubwa kwa Wamachinga kutambuliwa na Serikali pamoja na taasisi
zingine,” amesema Kandege na kuongeza…
“Mikopo
hii ni mfano halisi wa kizalendo na huu ni
ushindi mkubwa kwa Taifa, pia apongezwe JPM kwa kuanzisha vitambulisho hivi
vitakavyoibua wafanyabiashara mamilionea na bilionea.”
Kandege
ameziagiza halmashauri zote nchini kuwa, Kitambulisho vya Mjasiriamali ndiyo kiwe mojawapo ya vigezo vya kupata
mikopo ya halmashauri na manispaa kwa vijana, akina mama na wenye ulemavu.
Amewataka
Wakurugenzi wa halmashauri na manispaa zingine kwenda kujifunza Kigamboni jinsi ya kuanzisha mikopo kwa kutumia
Vitambulisho vya JPM. Ameiomba CRDB
kusambaza huduma hiyo ya mikopo nchi nzima pia kuongeza wigo kwa kuwakopesha mayaya,
wahudumu wa ndani (House girls/boys), madereva, wakulima, wavuvi na makundi
mengine ili kuwakomboa kiuchumi.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Abdulmajid Nsekela, amempongeza Rais John
Magufuli kwa kuanzisha Kitambulisho cha Mjasiriamali jambo ambalo limesaidia kuwarasimisha
kirahisi wafanyabiashara wanaosaidia kuinua uchumi wa nchi.
Amesema
CRDB ipo mstari wa mbele kuunga mkono mikakati ya maendeleo inayoanzishwa na
Serikali, ikiwemo ya wajasiriamali wenye vitambulisho vya JPM kwa kuwapatia
mikopo nafuu isiyo na riba wala dhamana.
Dk
Nsekela amesema kuwa CRDB ipo tayari kuwalea
vijana ambao ni asilimia kubwa ya wajasiriamali na wasiyo na ajira ili
wapate mitaji na kuwa wafanyabiashara wakubwa.
Amesema
kuwa Mkopo wa Jiwezeshe ambao ni mahususi kwa wajasiriamali wadogo, huinua
uwezo wa biashara kwa watu binafsi na vikundi. Mkopo huo unapatikana kupitia
simu za mkononi kwa wateja waliojisajili na huduma ya SimAccont kwa kupiga
*150*62# na kufuata maelekezo.
Unakopeshwa
kuanzia sh. 10,000 hadi sh. 500,000.
mkopo wa kuanzia sh. 10,000 – 50,000 akirejesha ndani ya miezi mitatu hulipa gharama ya mkopo
sh. 500 na mkopo wa sh. 50-150,000 hulipa gharama za mkopo sh 1,000 na kuanzia
sh. 150,000-500,000 gharama ni sh 2,000 tu. Mikopo hiyo haina dhamana.
mwisho

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇