Na.Khadija seif, Michuzi TV
MSANII
wa Bongofleva Nasib Abdul a.k.a Diamond platinum amewapongeza
wasanii,makampuni pamoja na vyombo vya habari kwa kufanikisha tamasha la
wasafi lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Diamond
amesema hayo katika ukumbi wa Hyatt regency uliopo jijini Dar es salaam
,nakugusia swala la wasanii hao kutoka nchi ya Nigeria kuwepo kwao
kulikua na lengo maalumu.
"Lengo
lilikua ni kujifunza kwa wenzetu jinsi ya kutumbuiza kwao kwa kuona
mubashara tofauti na wengi wetu tulikua tunaona tu kupitia televisheni
au kwenye mitandao ya kijamii,"
Aidha,mbali
na kujifunza kutoka kwa wasanii hao wawili Diamond amefafanua zaidi
kuwa wizkid na tiwasavage wataweza kututangaza kuanzia siku
walipofika,sehemu watakazotembelea ,hivyo kutaleta ushawishi kwa watu
ambao wanawatazama kutamani kufika nchi ya Tanzania.
Hata
hivyo amewaomba wadhamini mwakani msimu mwingine wa Tamash hilo
kuwaongezea fedha ili waweze kuwa na nafasi ya wasanii wengine kushiriki
kikamilifu.
"Japo
fedha ilikua pungufu sio sana lakini niliweza kutazama baadhi ya wasanii
kwa jicho la kipekee kutokana na mara nyingi kutopewa nafasi kwenye
majukwaa mbalimbali na ndio sababu pia sisi Kama wasafi na uongozi wa
lebo yetu Wcb kuwapa nafasi wakongwe wa Muziki akiwemo inspector
harun,Mandojo na domokaya,Madee na wengine kutumbuiza jukwaa la wasafi,"
Pia ametoa ushauri kwa wasanii kutosikiliza minong'ong'ono ya mashabiki zao wenye lengo la kuwagombanisha hasa mitandaoni.
"Wakati
mwengine Mashabiki zetu wanatufanya tugombane ,tuchukiane na hata
kutoelewana tuyapuuzie hayo kwani wote wanapenda kazi zetu kiujumla
akitokea kwenye tamasha langu ataimba nyimbo zangu na akija kwako
ataimba na zako huoni Kama wote Ni shabiki zetu tusiweke matabaka,"
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇