Na Amiri Kilagalila-Njombe
Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG Charles Kichere ameagiza watumishi wa serikali nchini kutumia pesa za serikali kwa maendeleo ya wananchi ili kukuza uchumi wa nchi na ustawi wa watu wake.
Kichere amesema serikali imekuwa ikitoa pesa nyingi kwa ajili ya miradi ya mingi ikiwemo ya maji,umeme na bara bara lakini miradi imekuwa ikishindwa kukamilika huku pesa imetolewa.
CAG Kichere ametoa maagizo hayo mkoani Njombe wakati akikabidhi ofisi kwa katibu tawala mpya wa mkoa huo Catarina Revocat huku akitolea mfano mkoa wa Njombe unaozungukwa na mito lakini bado kumekuwa na changamoto kubwa ya maji.
“Baada ya kufika huku Njombe nimejifunza mengi sana ukiwa serikali kuu huwezi kujua nini huku kinaendelea,lakini huku ndio maendeleo inatakiwa yatoke,serikali kuu imewekeza kwenye miradi mikubwa lakini huku kuna miradi midogo ya maji,umeme,barabara,afya pesa zinakuja,tuzitumie vizuri za pesa serikali zinazokuja ili tuwaletee wananchi maendeleo,nimeshuhudia pesa zinakuja lakini miradi haikamilika”anasema Charles Kichere
Aidha ameahidi kuelekeza ofisi ya mkaguzi ya taifa kuhakikisha wanafuatilia miradi yote ya maji iliyopo mkoani Njombe kuhakikisha imefanyika kikamilifu.
“Ni jambo la kusikitisha kidogo mkoa wa Njombe ambao umezungukwa na mito na mabonde mbali mbali kuna shida ya maji tatizo ni nini hasa,nitaelekeza wenzangu katika ofisi ya mkaguzi ya taifa wahakikishe wanafuatilia miradi yote ya maji mkoa wa Njombe tuhakikishe inafanyika vizuri na inawaletea manufaa wananchi wetu na tuhakikishe tunapata value for money”anasema tena Kichere
Bi.Katarina Tengia Revocati ni katibu tawala mpya wa mkoa wa Njombe mara baada ya kupokea ofisi hiyo ameahidi kufanya kazi kikamilifu kutokana na maelekezo ili kuyafikia mageuzi ya kiuchumi wananchi wa mkoa wa Njombe.
“Twende na mtazamo unaohakikisha mwananchi wa kawaida anaweza kufaidi yale mageuzi makubwa ya kiuchumi ambayo mh.Rais pamoja na uongozi mzima wa kitaifa wanayafanya”anasema Katarina
Nestory Karia ni mkaguzi wa hesabu za serikali kanda ya kusini,amesema ofisi ya mkaguzi itaendelea kushirikiana na ofisi ya katibu tawala katika kazi ili kuhakikisha hakuna halmshauri ya mkoa huo itakayoweza kupata hati chafu. Mkuu wa mko wa Njombe Christopher Ole Sendeka,amesema serikali imeendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika mkoa wa Njombe hivyo kazi yao ni kuhakikisha wanasimamia miradi hiyo.
“Tuna miradi mikubwa huku inayoendelea ukiacha hiyo ya bara bara,tuna soko la kisasa jampo kuna changamoto zake,tuna ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa ambayo inajengwa kwa jumla ya bilioni saba,tunapata fedha kwa ajili ya miradi inayowagusa wananchi, kazi yetu ni kuendelea kuhakikisha tunapata value for money”anasema Ole Sendeka
Novemba 3,2019 Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alifanya uteuzi wa viongozi mbali mbali akiwemo Bw.Charles Edward Kichere kuwa mdhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali akichukuwa nafasi ya Prof.Mussa Juma Assad amabye kipindi chake cha miaka 5 kilikwisha tarehe 04 Novemba 2019.
Kabla ya uteuzi Bw.Kichere alikuwa katibu tawala wa mkoa wa Njombe huku nafasi hiyo kwa sasa ikichukuliwa na Bi.Katarina Tengia Revocati aliyekuwa msajili mkuu wa mahakama ya Tanzania.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇