Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania imewaasa wananchi wa mikoa ya Kaskazini, Kilimanjaro Arusha na Manyara kufuatilia utabiri wa hali ya hewa unaotolewa kila siku na mamlaka hiyo ili kuweza kuepuka majanga yanayoweza kujitokeza.
Katika Taarifa iliyotolewa na Meneja wa kituo Kikuu cha utabiri TMA, Samwel Mbuya leo Oktoba Mosi, 2019 imesema leo majira ya mchana katika baadhi ya mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara kulitokea na upepo mkali uliotokana na mkusanyiko wa mawingu ya radi katika eneo dogo na kutengeneza mkondo wa mawingu.
"Mawingu hayo yalisababisha dhoruba ya upepo uliokuwa na kasi ya kilomita 50 kwa saa hali ambayo ilidumu kwa takribani dk.30 katika eneo husika kabla ya hali hiyo kurejea kawaida.
Taarifa hiyo imesema, mkondo huo wa mawingu ulianzia kusini mwa Kenya na kujielekeza katika baadhi ya mikoa hiyo na kufuatiwa na vipindi vya mvua na ngurumo kutokana na mawingu hayo.
Amesema, matukio hayo ni hali inayoweza kujitokeza panapotokea mawingu hayo mazito kujikusanya katika mkondo, hivyo amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kila siku na kuzingatia kufuatilia hali ya hewa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇