Na Rahma Khamis Maelezo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Zanzibar Iddi Haji Makame amewataka wananchi wa Kwahani kutokua na wasiwasi kwa kuvunjiwa nyumba zao kwani Serekali ina dhamira ya dhati ya kuwajengea nyumba bora na za kisasa
Ameyasema katika eneo litakalojengwa mji mpya wa nyumba za kisasa Kwahani wakati wa hafla ya kutiliana saini na Kampuni ya ujenzi wa nyumba hizo Estim Construction LTD ya Dar es salaam .
Amesema kuanza kwa ujenzi wa awamu ya kwanza ya nyumba tano za ghorofa nne kila moja na maduka eneo eneo la chini ni uamuzi wa Serekali wa kuwaondoshea wananchi mazingira ya zamani na kuwawekea ya kisasa.
Aliwaeleza wananchi wa Kwahani kwamba Kampuni iliyopewa kazi za ujenzi wa mji mpya Kwahani inauwezo mkubwa na wamekubaliana watakamilisha kazi hiyokwa kipindi cha mwaka mmoja.
Amewashauri kuendelea kuvuta subira katika kipindi hicho cha mpito huku wakiweka matumaini ya kuishi katika mazingira bora na yakisasa.
MsimamizI wa ujenzi wa nyumba hizo Lazaro Peter amewataka wnanchi wa eneo la Kwahani kutoa ushirikiano wakati wa ujenzi ili kazi ziweze kwenda kwa kasi na zikamilike kwa muda uliopangwa.
Aliwapa matumaini makubwa wananchi waliovunjiwa nyumba zao kwamba watapata nyumba bora na za kisasa katika kipindi cha muda mfupi ujao.
Sheha wa Shehia ya Kwahani Machano Mwadini Omar ameishauri Kampuni ya ujenzi wa nyumba hizo kuwatumia vijana wa eneo hilo katika kazi zisizohitaji utaalamu ili nao waweze kufaidika na mradi huo.
Alieleza kuwa nyumba zilizovunjwa kwa ajili ya kupisha ujenzi mpya zilikuwa na vijana wengi waliokuwa wakiendesha shughuli zao za maisha na hivi sasa hawana kazi maalum hivyo iwapo watapatiwa kazi wakati wa ujenzi zitawasaidia kimaisha
Baadhi ya wananchi waliovunjiwa nyumba Ali Hamad Haji na Hija Sudi Juma wamesema kuwa kuvunjiwa kwa nyumba zao imeleta shida kidogo lakini wataendelea kuvuta subira na kuitaka Serekali ifanye uadilifu wakati ujenzi utakapokamilika.
Aidha wameipongeza Serekali kwa hatua waliochukua ya kupatiwa mtaji wa kutafuta makazi ya muda huku wakisubiri makazi mapya ya kisasa yatakayowatoa katika hali ya unyonge.
Katika utiaji saini Serikali iliwakilishwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Iddi Haji Makame na Kampuni ya Estim Construction Co. LTD LTD iliwakilishwa na Meneja Mkuu wa Kampuni hiyo Girdhar Pindolia
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Iddi Haji Makame (kushoto)akitiliana saini na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ESTIM Construction co.ltd Girdhar M,Pindolia kuhusiana na Ujenzi wa Mji mpya wa Kwahani hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Iddi Haji Makame (kushoto)wakikabidhiana hati ya saini na Meneja Mkuu wa Kampuni ya ESTIM Construction co.ltd Girdhar M,Pindolia kuhusiana na Ujenzi wa Mji mpya wa Kwahani hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango Iddi Haji Makame (kushoto)akimkabidhi Ramani ya Ujenzi wa Mji Mpya kwahani Meneja Mkuu wa Kampuni ya ESTIM Construction co.ltd Girdhar M,Pindolia hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar.
Ramani ya Nyumba za Mji mpya kwahani utakaogharimu kiasi cha Shil,Bilioni miambili hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar.
Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria katika hafla ya utiaji saini Ujenzi wa Mji mpya wa Kwahani hafla iliofanyika muembe njugu Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇