LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 24, 2019

SERIKALI YA KENYA: HADI SASA WATU 29 WAMEPOTEZA MAISHA KUTOKANA NA MAFURIKO YA MVUA ZINAZO ENDELE KUNYESHA NCHINI

  • Serikali ya Kenya imethibitisha kufariki dunia watu 29 kutokana na mafuriko yanayotokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, watu wengine sita wanaendelea kuuguza majeraha kutokana na matukio hayo katika mikoa ya kati na Pwani ya Kenya.

Hali ya mafuriko maeneo ya Pwani

Aidha serikali ya Nairobi imesema kuwa, mvua hizo zimeharibu miundombinu kama vile barabara, madaraja yenye thamani kubwa ya fedha pamoja na makazi ya watu. Kufuatia hali hiyo, wakazi wanaoishi maeneo ya bondeni wametakiwa kuondoka katika maeneo hayo kwa ajili ya usalama wao.
Tujiunge na mwandishi wetu wa mjini Mombasa, Seifullah Murtadha kwa taarifa kamili………./

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages