LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 24, 2019

MKURUGENZI MTENDAJI MOI MGENI RASMI KATIKA BONANZA LA HISANI UWANJA WA UHURU DAR ES SALAAM

 Taasisi ya Mifupa (MOI) imeandaa mechi ya hisani ili kuchanga fedha kwa ajili ya watoto wenye vichwa vikubwa na mgongo wazi na wagonjwa waliotelekezwa na ndugu zao, Mechi hiyo ya kirafiki itazikutanisha timu machachari ya MOI na ile ya Hospitali ya Tasaktaa kutoka Zanzibar. Mechi itafanyika siku ya kilele cha Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Watoto wenye Vichwa Vikubwa na Mgongo wazi tarehe 25 Oktoba 2019. Mechi itafanyika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam, liingilio jukwaa kuu ni shilingi elfu tano na mzunguuko ni shilingi elfu tatu. ''Wananchi wote mnakaribishwa kushuhudia mechi safi kutoka kwa wataalam wa tiba mbalimbali. Lakini pia kuhudhuria kwao ni kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Taasisi ya MOI kutoa huduma bora kwa wahitaji''. Alisema Patrick Mvungi nahodha wa timu ya MOI ambao ndio waandaji wa mechi 
hiyo
 Mkurugezi Mtendaji Dkt. Respiucious Bonface 
akizungumza mara baada ya wataalam wa Tiba mbalimbali wa Timu ya Hospitali ya Tasaktaa kutoka Zanzibar kuwasili kwa maandalizi ya Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam Oktoba 25, 2019. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)




 Wachezaji wa Timu ya Hospitali ya Tasaktaa kutoka Zanzibar wakiingia katika ukumbi wa Mikutano MOI

 Wachezaji wa Timu ya Hospitali ya Tasaktaa kutoka Zanzibar wakiwa wanaingia katika ukumbi wa Mikutano MOI.
 Wachezaji wa Timu ya Hospitali ya Tasaktaa kutoka Zanzibar wakiwa katika Chumba cha Mkutano MOI
 Mkurugezi Mtendaji Dkt. Respiucious Bonface akizungumza jambo  na wachezaji wa Timu ya Hospitali ya Tasaktaa kutoka Zanzibar akiwa na baadhi ya viongozi wa Timu zote mbili

 Mkurugezi Mtendaji Dkt. Respiucious Bonface katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Hospitali ya Tasaktaa kutoka Zanzibar.
 Nahodha wa Timu ya MOI Patrick Mvungi akizungumza jambo leo mara baada ya Wataalam wa Tiba mbalimbali wa Timu ya Hospitali ya Tasaktaa kutoka Zanzibar kuwasili kwa maandalizi ya Mchezo huo utakaofanyika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam Oktoba 25, 2019.

 Wataalam wa Tiba mbalimbali wa Timu ya Hospitali ya Tasaktaa kutoka Zanzibar watembezwa sehem mbalimbali ikiwemo chumba cha Upasuaji na kujione utendaji wa kazi mahiri unaofanywa na Madaktari wa MOI 
Mkurugezi Mtendaji Dkt. Respiucious Bonface katika picha ya pamoja na wachezaji wa Timu ya Hospitali ya Tasaktaa kutoka Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages