LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 17, 2019

MIFUKO YA UWEZESHAJI KIUCHUMI YATAKIWA KUWAWEZESHA WANANCHI MITAJI WAANZISHE VIWANDA

 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) (aliyemwakilisha Mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka),  akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya Mifuko na programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  
katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.


Baadhi ya wananchi wa Bariadi mkoani Simiyu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (pichani hayupo) katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya Mifuko na programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) akimsikiliza Afisa kutoka Mamlaka ya Masoko ya  Mitaji na Dhamana, katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya Mifuko na programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga katika picha ya pamoja na baadhi 
ya viongozi  na Watumishi wa BarazalaTaifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi katika Maonesho ya tatu ya Mifuko na programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya 
kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
 Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (aliye vaa suti nyeusi) akimsikiliza mmoja wa wanufaika wa mikopo kutoka SIDO katika ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya Mifuko na programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) akizungumza jambo na  Afisa Uhusiano Mkuu wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi (NEEC), Bw. Edward Kessy (kulia) wakati alipotembelea mabanda ya maonesho wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya Mifuko na programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
  Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga(mwenye suti nyeusi) akiangalia bidhaa za wajasiriamli kutoka mikoa ya Tabora na Dodoma wakati alipotembelea mabanda ya maonesho wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya Mifuko na programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
Afisa Biashara wa Taasisi ya Private Agricultural Sector Support (PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Bariadi, Mhe. Festo Kiswaga (kushoto) alipotembelea mabanda ya maonesho wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya tatu ya Mifuko na programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.


Na Stella Kalinga, Simiyu RS
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mhe. Festo Kiswaga ametoa wito kwa Mifuko na programu 
za uwezeshaji wananchi kuangalia jinsi ya kuwezesha wananchi wengi zaidi kupata mitaji ya kuanzisha viwanda, ili uchumi wa nchi ukue na kupunguza changamoto zinazokabili jamii.

 Kiswaga ameyasema wakati akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka 
katika uzinduzi wa Maonesho ya tatu ya  Mifuko na programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, uliofanyika Oktoba 16, 2019  katika Uwanja wa Halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu.

“Sote tunafahamu kwamba Tanzania inalenga kufikia uchumi wa katika ifikapo mwaka 2025 
na viwanda ni nyenzo itakayowezesha nchi kufika huko; viwanda vina mchango mkubwa sana katika kukuza uchumi wa nchi  kwa kuwa vinanufaisha jamii kwa kutoa ajira, kulipa 
kodi, kununua malighafi kutoka kwa wakulima na mengine mengi,” alisema Kiswaga.

Aidha, Kiswaga alitoa wito kwa wananchi wa mikoa ya kanda ya ziwa na maeneo mbalimbali 
nchini kufika katika maonesho haya kupata maelezo kutoka kwa wawakilishi wa Mifuko na programu za uwezeshaji za Serikali, kuonesha bidhaa, kunua bidhaa za 
wajasiriamali na kupata uelewa wa masuala ya uwezeshaji wananchi.
Naye Afisa Maendeleo ya Biashara wa Taasisi ya kusaidia sekta binafsi na Kilimo,  

(PASS) Kanda ya Ziwa, Faustine Mungo amesema wameandaa mpango mkakati wa miaka 
mitano ambapo wanatarajia kutoa ajira 700,000 ambao unatarajia kuzifikia familia 
zaidi ya 200,000.

Kaimu Mkurugenzi wa Uwezeshaji na Ushiriki wa Watanzania katika Uwekezaji, Bi.Esther Mmbaga kutoka Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi Kiuchumi(NEEC), amesema malengo ya maonesho haya ni pamoja na kukuza uelewa wa wananchi  kuhusu uwepo, majukumu na vigezo katika kutoa huduma za mikopo na programu za uwezeshaji.

Bi. Mmbaga ameongeza kuwa malengo mengine ni kuhamasisha wananchi ili waweze 
kunufaika na fursa zilizopo katika mifuko na programu za uwezeshaji na kuhamasisha 
wananchi kujenga utamaduni wa kuweka akiba na kuwekeza katika miradi yenye tija.


Maonesho ya tatu ya  Mifuko na programu za uwezeshaji na vikundi vya kifedha  vya kijamii, yenye Kauli Mbiu “Mitaji ni Chachu ya Kujenga Uchumi wa Viwanda”ambayo 
yanaendelea katika uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi yanatarajiwa kufungwa rasmi 
Oktoba 20, 2019 

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages