LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 10, 2019

MCHAKATO KUOMBA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI KWA TIKETI YA CCM KATIKA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA NA VIJIJI MWAKA 2019

DODOMA, TANZANIA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesisitiza wale wote wanaoamini kuwa wamekidhi vigezo na masharti ya uanachama wa CCM, kujitokeza kuchukua fomu ili kuomba kuingia kwenye mchujo ili kuteuliwa kugombea katika  nafasi za uongozi katika Uchaguzi wa Serikali za mitaa na Vijiji uliopangwa kufanyika Novemba mwaka huu.

"Uongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) chini ya Mwenyekiti wa CCM Rais Dk. John Magufuli unasisitiza wale wote wenye sifa na wamekidhi vigezo na masharti ya uanachama wajitokeze kuchukua fomu na kuomba kufikiriwa na hatimaye kuteuliwa na kwamba fomu zinatolewa bure katika Matawi ya CCM", imesema  taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC), Itikadi na Uenezi, Humphrey Polepole, leo jijini Dodoma.

Taarifa hiyo imesema "Tunatoa rai kwamba Chama kinatarajia wana CCM wenye kuishi misingi ya Chama chetu watu mahodari wa uadilifu, uaminifu, unyenyekevu, Wachapa kazi, wenye kazi zinazowaletea kipato halali, watetezi wa kweli wa Maslahi ya wananchi, wanaochukizwa na rushwa na ubadhirifu wa mali za umma wajitokeze ili wakakamilishe safu ya uongozi wa Serikali ya CCM inayotoa uongozi na kuleta maendeleo makubwa kwa haraka katika nchi yetu chini ya Rais Dk. John Magufuli. 

Ufuatao ni mtiririko wa matukio ndani ya CCM  uliotolewa na Polepolea, ambao wanachama, viongozi na wanaoomba kuteuliwa na Chama wanapaswa kuuzingatia;-

NGAZI YA VIJIJI NA MITAA
Tarehe 7 – 12 Oktoba, 2019: Kuchukua na kurejesha fomu za kuomba kugombea Uenyekiti wa Mitaa, Vijiji na Ujumbe wa Serikali za Vijiji na Mitaa kwa Makatibu wa Matawi ya CCM kote nchini.

Tarehe 13 Oktoba, 2019: Kamati za Siasa za Matawi kujadili wagombea na kutoa Mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Kata

Tarehe 14 – 15 Oktoba, 2019: Kamati za Siasa za Kata kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Wilaya

Tarehe 16 – 18 Oktoba, 2019: Kamati za Siasa za Wilaya kujadili wagombea na kufanya uteuzi wa wagombea kwa ajili ya kupigiwa kura za maoni na Mkutano wa Wanachama wote wa Tawi.

Tarehe 19 – 20 Oktoba, 2019: Mikutano ya kura za Maoni ya nafasi ya Mwenyekiti wa Mtaa au Kijiji – Mkutano wa Wanachama wote wa Tawi

BAADA YA KURA ZA MAONI
Tarehe 21 Oktoba, 2019: Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu za Matawi kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu ya Kata

Tarehe 22 – 23 Oktoba, 2019: Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu za Kata kujadili wagombea na kutoa mapendekezo yake kwa Kamati za Siasa za Wilaya

Tarehe 24 – 26 Oktoba, 2019: Kamati za Siasa za Halmashauri Kuu za Wilaya kujadili wagombea na kutuma mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya.

Tarehe 27 – 28 Oktoba, 2019: Halmashauri Kuu ya CCM ya Wilaya Kufanya Uteuzi wa Mwisho wa Wanachama watakaogombea Uenyekiti wa Mtaa, Ujumbe wa Kamati ya Mtaa, Uenyekiti wa Kijiji na Ujumbe wa Halmashauri ya Kijiji.

NYONGEZA: RATIBA YA SERIKALI
 Tarehe 8 – 14 Oktoba, 2019: Zoezi la uandikishaji wapiga kura siku saba tu kwa Mwananchi mkaazi wa Mtaa/ Kijiji na Kitongoji 

Tarehe 29 Oktoba, 2019: Kuanza kuchukua fomu za kugombea

Tarehe 4 Novemba, 2019: Tarehe ya Mwisho ya kurejesha fomu kwa Msimamizi

Tarehe 10 Novemba, 2019: Uwasilishaji wa ratiba za kampeni kwa Msimamizi

Tarehe 17 – 23 Novemba, 2019: Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji

Tarehe 24 Novemba, 2019: Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Vijiji na Vitongoji

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages