LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 25, 2019

MAMA SALMA KIKWETE AUNGANA NA WANAWAKE VIOMGOZI MKUTANO WA KIMATAIFA BURUNDI

Mke wa Rais Mstaafu ambaye pia ni Mbunge wa Kuteuliwa, Mama Salma R Kikwete ameungana na Wanawake Viongozi mbalimbali kutoka Afrika katika Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake Viongozi unaofanyika nchini Burundi kuanzia tarehe 24-26 Octoba 2019

Mama Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA) anashiriki Mkutano huo wa siku 3 ambao umeanza Oktoba 24 na kufunguliwa na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza.
Mkutano huu umehudhuriwa na Mke wa Rais wa Burundi mwenyeji muandaaji Mama Denise NKURUNZIZA, Naibu Rais wa pili wa Bunge la nchi, Jocky Chantal NKURUNZIZA, na Kaimu Balozi wa Tanzania Nchini Burundi, Dr. Edmud Juma Kitokezi.

Viongozi wengine ambao wamehudhuria Mkutano huu ni pamoja na Naibu Karibu Mkuu UN anayeshughulikia maswala ya Afrika Mama Bintou Keita , Mke wa Rais wa Congo Brazaville Mama Antoinette Sassau Nguess. Mke wa Rais wa Central Africa Republic Madam Brigette Touadera.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages