Rais wa mwisho wa Umoja wa Sovieti amekutaja kupuuzwa sheria za kimataifa na kugeuzwa siasa za kimataifa na kuwa za kijeshi kuwa ndiyo hatari kubwa zaidi kwa dunia ya sasa.
Mikhail Gorbachev ameyasema hayo kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 30 tangu kusambaratika ukuta wa Berlin na kuongeza kuwa, vitisho, uingiliaji kati na mashambulizi ya kijeshi badala ya mazunumzo ya amani kwa ajili ya kuzipatia ufumbuzi hitilafu mbalimbali duniani, ni hatari kubwa inayomkabili mwanadamu.
Ameongeza kuwa, viongozi wa dunia wanakabiliwa na majukumu mengi mazito, na Marekani ambayo inadai kuwa kinara wa dunia ni nchi mfamo mbaya zaidi katika uwanja huo.
Rais huyo wa mwisho wa Umoja wa Sovieti ameashiria pia mkataba wa Silaha za Nyuklia za Masafa ya Kati (INF) na kusisitiza kuwa: "Tulikosolewa katika ngazi mbalimbali kwa kusaini mkataba huo, lakini Rais wa Marekani ametangaza kujitoa nchi hiyo kwenye mkataba huo."
Tarehe Pili Agosti mwaka huu Marekani ilitangaza kujitoa katika mkataba wa INF, na Russia pia ikajibu hatua hiyo ya Washington kwa kuuweka kando mkataba huo.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇