LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 10, 2019

DKT. KIGWANGALLA: MITANDAO YA MAJANGILI IMESAMBARATISHWA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema mitandao ya ujangili imesambaratishwa na hivyo kufanya ujangili wa kibiashara kwa meno ya tembo na faru kupungua kwa asilimia 80.

Ameitoa Kauli hiyo akiwa katika Kituo cha Mafunzo ya Awali ya Jeshi Usu Mbulumbulu kinachomilikiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kilichopo wilayani Karatu mkoani Arusha.

Akifunga mafunzo ya awali ya Jeshi la Usu kwa askari 112 wa NCAA Kigwangala amesema ujangili umekwishakoma nchini kwani kesi wanazopata ni za meno ya tembo waliouawa miaka nane hadi 10 nyuma na kwa upande wa faru hawapati kabisa.

“Hakuna tembo wapya wanaouawa, mitandao yao tumeisambaratisha. nina uhakika tukichukua takwimu uwezekano mkubwa ujangili utakuwa umepungua kwa zaidi ya asilimia 80,” amesema Dk. Kigwangala.

Ameongeza kuwa asilimia 20 inayobakia kati ya 80 huenda ikawa kwa wanyamapori wanaovamiwa kwa bahati mbaya, uwindaji haramu wa nyama ya kitoweo na kuwekewa sumu wanapovamia mashamba ya watu.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages