LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Oct 21, 2019

AZAM FC YAMRUDISHA ARISTICA CIOABA CHAMAZI COMPLEX



 Kocha mpya wa Azam FC, Aristica Cioaba, akiwa sambamba na mtangulizi wake, Etienne Ndayiragije, anayekwenda kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'. Wawili hao wamekutana makao makuu ya Azam FC (Azam Complex) wakiwa pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat', kukabidhiana kijiti, ikiwemo Ndayiragije kuwaaga wachezaji na kwenda kwenye majukumu yake mapya ya timu ya Taifa.
 Kocha mpya wa Azam FC, Aristica Cioaba, akitia saini mkataba wa mwaka mmoja wa kukinoa kikosi hicho akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'
Kocha mpya wa Azam FC, Aristica Cioaba, akitia akibidhiana mkataba wa mwaka mmoja wa kukinoa kikosi hicho akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin 'Popat'


Habari Kamili
Na Zainab Nyamka
UONGOZI wa Timu ya Azam FC imemtangaza Kocha aliyewahi kukinoa kikosi cha matajiri hao wa Chamazi,  Aristica Cioaba kuja kuchukua mikoba ya Etienne Ndayiragije.

Cioaba aliwahi kuifundisha kikosi hicho kabla ya kitimuliwa ila amerejea tena na kupewa mkataba wa mwaka mmoja.

Kocha huyo  anachukua mikoba ya aliyekuwa Kocha wa Azam, Etienne Ndayiragije, ambaye anatarajia kutangazwa kama Kocha Mkuu wa kudumu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars'.

Kocha huyo raia wa Romania, aliyewahi kuinoa Azam FC misimu miwili iliyopita, ataanza majukumu yake mara moja tutakapokamilisha taratibu za vibali vyake vya kufanya kazi nchini.

Aidha, kama ilivyokuwa awali Cioaba, mwenye leseni ya juu ya ukocha ya UEFA Pro Licence, amerejea sambamba na Kocha wa viungo, Costel Birsan, aliyekuwa naye awali kipindi anaifundisha Azam FC.

Mara baada ya kuingia mkataba rasmi mapema leo Jumatatu, Cioaba ameishukuru Bodi ya Wakurugenzi na uongozi mzima wa Azam FC kwa kuendelea kuwa na imani naye.

 "Naushukuru uongozi wa Azam FC kwa kuendelea kuwa na imani na mimi, kikubwa mimi sio mgeni hapa naijua timu, wachezaji wananijua na pia wanafahamu falsafa yangu, jambo kubwa ni kuendelea kuifanya timu kuwa juu pamoja na kushinda mataji," amesema.

Ndayiragije anaenda timu ya Taifa, baada ya Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC kuridhia ombi la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wanaomuhitaji awe kocha mkuu wa kudumu baada ya kufanya vizuri akiwa na kikosi hicho akiwa kocha wa muda.

Azam FC tunamtakia kila la kheri, Ndayiragije katika majukumu yake mapya akiwa Taif Stars, ambapo tutakuwa naye sambamba pale atakapohitaji kutoka kwetu msaada kwenye masuala yake kiufundi.

No comments:

Post a Comment

ANDIKA MAONI (COMMENTS) HAPO👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages