Serikali kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama, imewataka wanawake kuwa na kiherehere cha maendeleo katika utendaji kazi wao wa kila siku ili mchango wao utambulike.
Jenista ameyasema hayo jijini Dar es Salaam, wakati wa mkutano mkuu wa pili wa viongozi wanawake na utoaji tuzo kwa wanawake walioshiriki mafunzo ya mkakati wa kuwawezesha kiuongozi, inayosimamiwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE), alisema anakerwa na unyonge wa wanawake.
Hata hivyo alishangazwa wanawake wakandarasi wanafanya kazi kubwa, lakini hawaonyeshi jitihada kama wanaume.
“Nilishangazwa kuona wakandarasi wanawake wamefanya kazi nyingi kubwa, wanasema wanaume wao ndio wana kiherehere, wanajitokeza zaidi kila tukio tofauti na sisi, jambo hilo silitaki, naomba tuwe na kiherehere cha kuelezea mazuri yetu,” alisema Jenista.
Alisema wakati sasa umefika wanawake kujipima mafanikio yao na kuangalia wanakosea wapi, pia wawe na kiherehere ili waweze kuheshimika ndani ya jamii.
Jenista alisema atahakikisha anasimamia mazingira ya wanawake kwa kuweka sera nzuri za jinsia wakati wa mapitio ya sera ya ajira ya mwaka 2008 ili kuinua ushiriki wa wanawake katika nafasi mbalimbali.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇