LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 20, 2019

Waziri Mpina Awataka Wafugaji Kuongeza Uzalishaji wa Maziwa Nchini



Waziri wa Mifugo na  Uvuvi Luhaga Mpina amewataka wafugaji kuongeza uzalishaji wa maziwa nchini ili kuchochea uwekezaji katika Tasnia ya Maziwa.

Hayo amesema jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na  waandishi wa habari kuelekea siku ya unywaji maziwa shuleni Duniani itakayoadhimishwa Septemba 25 mwaka huu  mkoani Iringa.

Mpina amesema kuwa ni mikakati ya serikali kuhakikisha kuwa uzalishaji wa maziwa unaongezeka kutoka lita bilioni 2.7 hadi kufika lita bilioni 7 kwa mwaka ifikapo 2020.

Amesema kuwa  malengo ya serikali ifikapo mwaka 2025 kila shule ya msingi iwe na  programu za kunywa maziwa shuleni na kila mtanzania awe anakunywa angalau  lita 100 kwa mwaka.

Kwa sasa kuna shule 25 tu ambazo zinatekeleza Programu ya unywaji maziwa shuleni na  kunufaisha jumla ya wanafunzi16.849 kwenye wilaya za Njombe, Mbeya na Wangingo'mbe.
Programu hizi zinaendeshwa kwa ushirikiano na  Mamlaka za Serikali za Mitaa, Viwanda vya kusindika maziwa, wazazi na wafadhili mbalimbali.

Waziri Mpina ametoa pia rai kwa wananchi kunywa maziwa na bidhaa za maziwa ili kuchochea maendeleo ya Tasnia ya Maziwa.

Maadhimisho ya Siku ya Unywaji Maziwa shuleni yanatarajiwa kufanyika mkoani Iringa uwanja wa Samora. Kauli Mbiu ya Maadhimisho haya ni Glasi moja ya maziwa kila siku kwa afya na  Elimu bora.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Kupanga Mpina akizungumza na waandishi habari kuhusiana maadhimisho ya Siku ya unywaji wa Maziwa yatakayofanyika mkoani Iringa.

No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages