Takribani wanajeshi 128,000 kutoka mataifa nane ya mashariki watashiriki katika mafunzo makubwa ya kijeshi nchini Urusi na mataifa ya Asia ya kati.
Mafunzo hayo yalianza siku ya Jumatatu nchini Urusi, Kazakhstan na Tajikistan na yanatarajiwa kukamilika siku ya Jumamosi.
Mazoezi hayo huandaliwa na Urusi kila mwaka, ingawa mwaka huu imeshirikisha China, India, Pakistan, Kazakhstan, Kyrgyzstan, Tajikistan na Uzbekistan.
Inaripotiwa kuwa zaidi ya vitengo 20,000 vya silaha za kijeshi, ndege 600 na meli za vita 15 zitashiriki katika zoezi hilo.

No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇