Wizara ya afya nchini Ufaransa yatangaza vifo vya watu 1435 kutokana na joto kali mwaka 2019.
Wizara ya afya nchini Ufaransa yatangaza vifo vya watu 1435 vilivyotokea kufuati joto kali katika msimu wa kiangazi mwaka 2019.
Joto kali nchini Ufaransa limeripotiwa katika nyakati mbili, ya kwanza ikiwa kati ua Juni 24 na Julai 7 huku ya pili ikiripotiwa kati Julai 21 na Julia 27.
Joto kali limesababisha vifo vya watu 1435 kote nchini Ufaransa.
Idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na watu waliofariki mwaka 2003.
Wizara ya afya ya Ufaransa imetangaza kuwa kiwango cha joto mwaka 2019 katika msimu wa kiangazi kimeongezeka na kufikia nyuzi joto 46 katika eneo la Kusini-Magharibi.
Rika la watu wenye umri wa kuanzia miaka 75 ndio walioathirika kwa kiasi kikubwa.
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇