Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Iddi akitoa hotuba ya kufunga rasmi Tamasha la Nne la Sanaa na Utamaduni la Jumuiya ya Afrika Mashariki (JAMAFEST ) lililofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia tarehe 21 hadi 28 Septemba 2019. Tamasha hilo la aina yake lilizishirikisha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiwemo Burundi, Rwanda, Kenya, Uganda na Tanzania. Wakati wa Tamasha hilo vikundi mbalimbali vya sanaa na utamaduni kutoka nchi hizo vilishiriki. Katika hotuba yake Mhe. Balozi Iddi alitoa rai wadau wa sanaa na utamaduni kujikita kwenye ubunifu kwa ajili ya kukuza uchumi kupitia sanaa. Tamasha la JAMAFEST ambalo hufanyika kila baada ya miaka miwili limepangwa kufanyika mwaka 2021 nchini Burundi |
No comments:
Post a Comment
MAONI (COMMENTS)👇