LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 5, 2019

RIPOTI YA UN: MAREKANI, UINGEREZA NA UFARANSA ZINAHUSIKA KUTENDA JINAI ZA KIVITA NCHINI YEMEN

Uchunguzi mpya uliofanywa na timu ya wataalamu wa Umoja wa Mataifa umeeleza kuwa, kutokana na kuusaidia muungano wa Saudia kwa taarifa za kiintelijensia na kilojistiki, Marekani, Ufaransa na Uingereza ni washirika wa utendaji uhalifu wa jinai za kivita dhidi ya Yemen ikiwemo kuihilikisha nchi hiyo masikini ya Kiarabu kwa njaa, kama mbinu mojawapo ya kijeshi.
Uchunguzi huo wa kimataifa umeubebesha lawama rasmi muungano wa Saudia na waungaji mkono wake, za mauaji ya raia wa Yemen yaliyofanywa kwa mashambulio ya anga na kuiwekea nchi hiyo mzingiro wa pande zote uliosababisha kutokea baa la njaa ambalo halijawahi kushuhudiwa nchini humo.
Watoto ni waathirika wakubwa zaidi wa baa la njaa lililotokea Yemen kutokana na mzingiro uliowekwa na Saudia na washirika wake
Ripoti ya wachunguzi wa Umoja wa Mataifa vile vile imeonyesha kutiwa wasiwasi na utendaji kazi kiupendeleo wa tume ya Saudia ya kuchunguza ukiukaji haki za binadamu na mauaji ya raia nchini Yemen.
Uwekaji watu kizuizini kinyume cha sheria, utesaji, ubakaji na kuuliwa wapinzani katika jela za kutisha zilizo chini ya vikosi vya jeshi la Imarati nchini Yemen, ni miongoni mwa jinai zingine zilizoashiriwa kwenye ripoti ya wachunguzi hao wa Umoja wa Mataifa.
Kuna nyaraka na ripoti mbali mbali zilizotolewa hadi sasa ambazo zinaonyesha kuwa, kwa kuuzia silaha muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudia, Marekani na nchi za Ulaya ikiwemo Uingereza na Ufaransa zimehusika waziwazi na mauaji ya wananchi wasio na hatia wa Yemen.../

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages