LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 12, 2019

NAIBU SPIKA WA BUNGE LA TANZANIA AHIMIZA USAWA WA JINSIA KATIKA UONGOZI

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Naibu Spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Akson amesema kuwa, serikali isipoweka mazingira  rafiki kwa wanawake ikiwemo uhamasishaji  katika chaguzi Mbalimbali zijazo jambo la wanawake kushika nyadhifa mbalimbali  halitowezekana  kamwe.

Naibu Spika, Dkt Tulia ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati wa Kongamano mahususi la kuongeza ushirikiano kati ya Watunga sera na  Asasi za Kiraia yenye Lengo la kukuza usawa wa Kijinsia nchini.

Wakati wa kongamano hilo, Dkt Tulia amekiri uwepo wa vikwazo mbalimbali katika kumfanya mwanamke kufikia malengo, na kudai kuwa zipo juhudi  zinazofanywa na bunge la Tanzania ili kuhakikisha kuwa wanawake  hawaachwi nyuma ifikapo mwaka 2030.
Awali Mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali nchini Tanzania Women wake up  (WOWAP) lililopo Mkoani Dodoma  ambaye pia ni Mbunge wa viti maalum Fatma Toufiq amesema  kuwa nafasi za uongozi  hazina hati miliki hivyo kila mmoja naruhusiwa kugombea.

Hata hivyo,lengo la kongamano hilo ni kuimarisha ushirikiano kati ya watoa maamuzi ,na makundi ya wanawake ili kuwawezesha wanawake na wasichana kushiriki katika ngazi mbalimbali za uongozi na maamuzi.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages