Sep 17, 2019

'KUSHAMBULIWA VITUO VYA MAFUTA VYA SAUDIA, KUNABAINISHA UDHAIFU NA KUSHINDWA KWA RIYADH'

Michael Lodgers, ameyasema hayo katika mahojiano na kanali ya Deutsche Welle ya Ujerumani na kuongeza kwamba, wanachama wa harakati ya wananchi ya Answarullah nchini Yemen, ndio waliohusika katika shambulizi hilo kwenye taasisi za mafuta za Saudia. Sambamba na kupinga madai yanayotolewa dhidi ya Iran, Lodgers ameongeza kuwa ni kinyume na madai ya Mike Pompeo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kwamba, Tehran iko nyuma ya hujuma hiyo huko Saudia.
Sehemu ya ndege za Answarullah ya Yemen zinazoishambulia Saudia
Mtaalamu na mchambuzi huyo wa Ujerumani wa masuala ya Asia Magharibi amesisitiza kwamba shambulizi hilo lililoathiri sekta ya uzalishaji mafuta nchini Saudi Arabia, ni fedheha kwa Riyadh, kwa kuwa utawala wa Aal-Saud ni mnunuzi mkubwa wa silaha za Marekani. Jumamosi iliyopita, kikosi cha ndege zisizo na rubani kwa kushirikiana na kamati za wananchi, kilirusha ndege 10 zilizotengezwa na Wayemen, na kushambulia vituo vya kusafishia mafuta vya Buqayq na Khurais, vinavyomilikiwa na Shirika la Kitaifa la Mafuta la Saudia ARAMCO na kusababisha hasara kubwa kwa Riyadh.

No comments:

Post a Comment

MAONI (COMMENTS)👇

Post Top Ad

Pages