LATEST HEADLINES👉

Your Ad Spot

Sep 26, 2019

KAIMU MSAJILI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA WAAJIRI AFUNGA SEMINA YA VIONGOZI NA WATENDAJI WA TUGHE

  Kaimu Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania, Pendo Berege  akizungumza jambo wakati  akifunga Semina ya Viongozi na Watendaji wa TUGHE katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya leo Septemba 26, 2019.(PICHA NA KHAMISI MUSSA).

Nianze kwa kuwapongeza TUGHE kwa kuwa mfano kwa kuwapa Semina ya mafunzo wanachama wenu hongereni sana kwa elimu mnayowapa wanachama.


Akizungumza katika Semina ya Viongozi na Watendaji wa TUGHE katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya leo Septemba 26, 2019 Kaimu Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania, Pendo Berege alisema;.


Napenda kumshukuru Mungu kwa kunifikisha katika Semina hii ambayo nimeelezwa mmejadiliana maswala mbalimbali  na sisi kama Msajili wa vyama kwa kweli tumefarijika sana, kwanza kwa Chama kuona umuhimu wa kuwaelimisha wanachama wake.


 Chama kimeona umuhim wa kuwaelimisha wanachama wake katika nyanja Mbalimbali hongereni sana TUGHE .


Ndugu wanasemina naomba nisiendelee kuwachosha lakini nashukuru kwa sababu hii ndio fulsa yangu ya kwanza  tangu nishike nafasi hii kukutana na mkusanyiko wa wanachama wengi kama ninyi.


Lakini mmeeleza mmepata mafunzo kuhusu Utawala Bora, Uwajibikaji mahala pa kazi kukuza tija mahala pa kazi na masuala ya namna ya kupunguza migogoro mahala pa kazi na masuala ya afya hayo yote kama mmeyafuatilia kwa uzuri  mnairahisishia Ofisi ya Msajili ambapo Mwenyekiti wa Semina alivyosema kwamba mmepewa Shule.


Ninaomba Shule hii tuifikishe kwa wanachama ambao hawakuweza kupata nafasi ya kuwa pamoja nasi hapa Mbeya alisema Berege;.


Yote haya yatumike kwenye kile kikao chetu kitakacho toa dozi hii kwanza watatuelea sana kuona Mbeya tumekaa wiki nzima na pia wataona umuhimu wa kuchangia michango yao na nisisiza kwani mnairahisishia utekelezaji wa majukumu Ofisi ya Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania na ninajuwa mmeelewa nini maana ya Chama cha wafanyakazi.


Kunadhana ya wa waajiri kukataa vyama vya wafanyakazi mahala pa kazi, wengi wanasema vitaleta migogoro lakini ninyi mkawe mablozi wazuri kwa waajiri wengine na niimni yangu mtaongeza ufanisi.


Mfano mmeuona hapa katika Chama cha TUGHE niwashukuru sana na basi ushirikiano huo uwende ukaboreshe ili tusiendelee kupata vyama vinavyoomba kusajiliwa tuumiza pale ofisini.


Mtaji mkubwa wa Chama ni wanachama pia nieleze Sheria ya ajira na mahusiano kazini naimeeleza na imetoa fulsa sasa umoja wetu ndio utakao tuunganisha tulenge katika kukijenga chama chetu, tukipe nguvu na tukisaidie na kama kunachangamoto tuzitatue na kuzitafutia maja

wabu.

Tunapokuwa katika vyama tusijisahu kuwa sisi ni waajiriwa wasehem fulani na niseme na viongozi nabaada ya kusema hayo niwatakie kila la heri na niwatakie safari njema asanteni sana .

 Katibu TUGHE Mkoa wa Dodoma Mchenya John (kushoto)  akimueleza jambo na Kaimu Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania, Pendo Berege ambapo alikuwa mgeni rasmi katika Semina hiyo ya Viongozi na Watendaji wa TUGHE katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya leo Septemba 26, 2019.
  Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi Tabu Mambo akizungumza jambo wakati wa Semina iliyoandaliwa na Chama hicho Ukumbi wa Mkapa  Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
 Mwenyekiti wa Semina Ibrahim Mmbaga akitoa utambulisho kwa baadhi ya viongozi katika ukumbi wa Mkapa uliopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania Pendo Berege 
 Semina hiyo iliyoanza 23-26 katika Ukumbi wa Mkapa uliopo katika Halmashauri ya Jiji la hilo.
 Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Kaimu Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania kufunga Semina, Pendo Berege
Mwenyekiti TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Mziwanda Chimwege akizungumza jambo



 Washiriki wa Semina

 Baadhi ya viongozi wakiwa katika Semina hiyo

 Baadhi ya viongozi kutoka Tawi la Muhimbili Mloganzila

  Afisa Muuguzi Mwandamizi Damu Salama Kanda ya Nyanda Kusini akimtoa Damu Mwenyekiti wa Semina ya Viongozi na Watendaji wa TUGHE kabla ya mafunzo hayo kufungwa ambayo yalitanguliwa kwa kutolewa huduma bure bila mlipo kwa magonjwa kama, upimaji wa hiyari wa VVU, Upimaji wa magonjwa ya Sukari, plesha, nakufuatiw na uchangiaji wa Damu katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya leo Septemba 26, 2019.











  Naibu Katibu Mkuu TUGHE Jane Mbura  akitoa shukurani wa Waajiri, wawakilishi wa wafanya kazi na viongozi mbali mbali na Makatibu wa mabaraza nichukue nafasi hii kwaniaba yenu ninyi nyote na kwaniaba yangu kumshukuru Mgeni rasmi kwa namna ambavyo amekuja na kukubari kufunga Semina hii

Ndugu mgeni rasmi kwa kweli tunapenda kukushukuru sana kwa kutudhamini na kuja kuungana nasi katika kuhitimisha Semina hii pia tunakushukuru kwa ushirikiano wako unao tuonyesha katika vyama vya wafanyakazi na hasa TUGHE


Najuwa tumetoka mbali katika chama cha TUGHE na amekuwa mshauri na amekuwa muwazi kwa kila mtu na umetuasa, napenda nikuhakikishie kwamba washiriki hawa wa Semina umetuomba Elimu hii kuipeleka matawini






No comments:

Post a Comment

Tupia Comments👇

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages