Kaimu Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania, Pendo Berege akizungumza jambo wakati akifunga Semina ya Viongozi na Watendaji wa TUGHE katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya leo Septemba 26, 2019.(PICHA NA KHAMISI MUSSA).
Nianze kwa kuwapongeza TUGHE kwa kuwa mfano kwa kuwapa Semina ya mafunzo wanachama wenu hongereni sana kwa elimu mnayowapa wanachama.
Akizungumza katika Semina ya Viongozi na Watendaji wa TUGHE katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya leo Septemba 26, 2019 Kaimu Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania, Pendo Berege alisema;.
Napenda kumshukuru Mungu kwa kunifikisha katika Semina hii ambayo nimeelezwa mmejadiliana maswala mbalimbali na sisi kama Msajili wa vyama kwa kweli tumefarijika sana, kwanza kwa Chama kuona umuhimu wa kuwaelimisha wanachama wake.
Chama kimeona umuhim wa kuwaelimisha wanachama wake katika nyanja Mbalimbali hongereni sana TUGHE .
Ndugu wanasemina naomba nisiendelee kuwachosha lakini nashukuru kwa sababu hii ndio fulsa yangu ya kwanza tangu nishike nafasi hii kukutana na mkusanyiko wa wanachama wengi kama ninyi.
Lakini mmeeleza mmepata mafunzo kuhusu Utawala Bora, Uwajibikaji mahala pa kazi kukuza tija mahala pa kazi na masuala ya namna ya kupunguza migogoro mahala pa kazi na masuala ya afya hayo yote kama mmeyafuatilia kwa uzuri mnairahisishia Ofisi ya Msajili ambapo Mwenyekiti wa Semina alivyosema kwamba mmepewa Shule.
Ninaomba Shule hii tuifikishe kwa wanachama ambao hawakuweza kupata nafasi ya kuwa pamoja nasi hapa Mbeya alisema Berege;.
Yote haya yatumike kwenye kile kikao chetu kitakacho toa dozi hii kwanza watatuelea sana kuona Mbeya tumekaa wiki nzima na pia wataona umuhimu wa kuchangia michango yao na nisisiza kwani mnairahisishia utekelezaji wa majukumu Ofisi ya Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania na ninajuwa mmeelewa nini maana ya Chama cha wafanyakazi.
Kunadhana ya wa waajiri kukataa vyama vya wafanyakazi mahala pa kazi, wengi wanasema vitaleta migogoro lakini ninyi mkawe mablozi wazuri kwa waajiri wengine na niimni yangu mtaongeza ufanisi.
Mfano mmeuona hapa katika Chama cha TUGHE niwashukuru sana na basi ushirikiano huo uwende ukaboreshe ili tusiendelee kupata vyama vinavyoomba kusajiliwa tuumiza pale ofisini.
Mtaji mkubwa wa Chama ni wanachama pia nieleze Sheria ya ajira na mahusiano kazini naimeeleza na imetoa fulsa sasa umoja wetu ndio utakao tuunganisha tulenge katika kukijenga chama chetu, tukipe nguvu na tukisaidie na kama kunachangamoto tuzitatue na kuzitafutia maja
wabu.
Tunapokuwa katika vyama tusijisahu kuwa sisi ni waajiriwa wasehem fulani na niseme na viongozi nabaada ya kusema hayo niwatakie kila la heri na niwatakie safari njema asanteni sana .
Katibu TUGHE Mkoa wa Dodoma Mchenya John (kushoto) akimueleza jambo na Kaimu Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania, Pendo Berege ambapo alikuwa mgeni rasmi katika Semina hiyo ya Viongozi na Watendaji wa TUGHE katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya leo Septemba 26, 2019.
Katibu wa TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Bi Tabu Mambo akizungumza jambo wakati wa Semina iliyoandaliwa na Chama hicho Ukumbi wa Mkapa Halmashauri ya Jiji la Mbeya.
Mwenyekiti wa Semina Ibrahim Mmbaga akitoa utambulisho kwa baadhi ya viongozi katika ukumbi wa Mkapa uliopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambapo mgeni rasmi alikuwa Kaimu Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania Pendo Berege
Semina hiyo iliyoanza 23-26 katika Ukumbi wa Mkapa uliopo katika Halmashauri ya Jiji la hilo.
Mwenyekiti TUGHE Taifa, Archie Mntambo akizungumza jambo kabla ya kumkaribisha Kaimu Msajili wa vyama vya wafanyakazi na Waajiri Tanzania kufunga Semina, Pendo Berege
Mwenyekiti TUGHE Mkoa wa Dar es Salaam Mziwanda Chimwege akizungumza jambo
Washiriki wa Semina
Baadhi ya viongozi wakiwa katika Semina hiyo
Baadhi ya viongozi kutoka Tawi la Muhimbili Mloganzila
Afisa Muuguzi Mwandamizi Damu Salama Kanda ya Nyanda Kusini akimtoa Damu Mwenyekiti wa Semina ya Viongozi na Watendaji wa TUGHE kabla ya mafunzo hayo kufungwa ambayo yalitanguliwa kwa kutolewa huduma bure bila mlipo kwa magonjwa kama, upimaji wa hiyari wa VVU, Upimaji wa magonjwa ya Sukari, plesha, nakufuatiw na uchangiaji wa Damu katika Ukumbi wa Mkapa uliopo Halmashauri ya Jiji la Mbeya leo Septemba 26, 2019.
Naibu Katibu Mkuu TUGHE Jane Mbura akitoa shukurani wa Waajiri, wawakilishi wa wafanya kazi na viongozi mbali mbali na Makatibu wa mabaraza nichukue nafasi hii kwaniaba yenu ninyi nyote na kwaniaba yangu kumshukuru Mgeni rasmi kwa namna ambavyo amekuja na kukubari kufunga Semina hii
Ndugu mgeni rasmi kwa kweli tunapenda kukushukuru sana kwa kutudhamini na kuja kuungana nasi katika kuhitimisha Semina hii pia tunakushukuru kwa ushirikiano wako unao tuonyesha katika vyama vya wafanyakazi na hasa TUGHE
Najuwa tumetoka mbali katika chama cha TUGHE na amekuwa mshauri na amekuwa muwazi kwa kila mtu na umetuasa, napenda nikuhakikishie kwamba washiriki hawa wa Semina umetuomba Elimu hii kuipeleka matawini
Your Ad Spot
Sep 26, 2019
Home
featured
habari picha
KAIMU MSAJILI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA WAAJIRI TANZANI AFUNGA SEMINA YA VIONGOZI
KAIMU MSAJILI WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA WAAJIRI TANZANI AFUNGA SEMINA YA VIONGOZI
Tags
featured#
habari picha#
Share This
About khamisimussa77@gmail.com
habari picha
Tags
featured,
habari picha
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment
Tupia Comments👇